WINGU LA HABARI
NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeingia makubaliano ya
ushirikiano wa biashara na Kampuni ya Simu za mikononi ya Tigo Tanzania yatakayowezesha
wateja wa taasisi hizo kubadilishana fedha na huduma za fedha kupitia simu zao
za mkononi.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika ghafla ya kutangaza
ushirikiano huo, Mkuu wa Huduma za TTCL Pesa Bw. Moses Alphonce, amesema wamefanya hivyo ili kuhakikisha wanawapa
wananchi huduma bora ya fedha mitandaoni pamoja na kuunga mkono jitihada za
serikali.
Bw. Alphone amesema kuwa ushirikiana na tigo pesa na TTCL Pesa umelenga kuwapa
wananchi suluhisho sahihi la mahitaji yao ya kifedha ikiwa ni kuunga mkono
jitihada za serikali ya awamu ya tano za kusogeza huduma karibu zaidi na
watanzania.
“TTCL imeazimia kuwapa wananchi huduma za kiwango cha juu na cha ubora na
unafuu wa gharama za kupokea na kufanya miamala kwa kutumia simu zao pamoja na kuongeza
usalama na ufanisi wa shughuli za kiuchumi na kijamii.” amesema Bw. Alphonce.
Ameeleza kuwa TTCL Pesa inaendelea kujivunia uwezo wa hali ya juu katika
kutoa huduma bora na nafuu pamoja na kujidhatiti katika kutoa huduma kwa haraka
na usalama wa hali ya juu wa fedha za wateja.
Hatua hiyo ni mwendelezo wa jitihada za Shilika la Mawasiliano Tanzania ili kuhakikisha
inaongoza katika kutoa huduma bora katika soko la huduma la mawasiliano hapa
nchini.
“TTCL imeendelea kuwa mhimili Mkuu wa Mawasiliano hapa nchini katika
kutoa huduma za za data kwa taasisi za umma na binafsi pamoja na huduma za simu za mezani na
viganjani” amesema Bw. Alphonce.
Akizungumzia makubaliano hayo ya kibiashara Mkuu wa Huduma za Tigo pesa Bw. Hussein Saidi, amesema kuwa Tigo pesa imeendelea kufikisha huduma sehemu mbalimbali ambazo huduma za kifedha hazipatikani ili kuwawezesha watu kufanya huduma zao kutoka tigo kwenda TTCL Pesa.
Hata hivyo hatua hii ya makubaliano kati ya TTCL na Tigo ni muendelezo wa
jitihada za shirika la Mawasiliano Tanzania kurejea kwa kishindo katika soko huduma
za mawasiliano nchini, kwani hadi sasa TTCL imefanikiwa kufikisha huduma
za 4G lite kutoka mikoa 16 ya Tanzania bara na Visiwa vya Pemba na Unguja.
No comments:
Post a Comment