UNESCO YAWAJENGEA UWEZO WADAU NAMNA YA KUTUZA URITHI WA DIGITALI - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, March 29, 2018

UNESCO YAWAJENGEA UWEZO WADAU NAMNA YA KUTUZA URITHI WA DIGITALI

Washiriki wa semina iliyoandaliwa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wakiendelea kupewa elimu kuhusu namna ya kutuza urithi wa digital.
 Muhifadhi wa Urithi na Utamaduni kutoka Makumbusho ya Taifa Dkt Amandus Kweka.  
Washiriki wa Semina wakiwa katika picha ya pamoja.
WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni nchini Tanzania (UNESCO) , limewataka watanzania kutumia vyema mfumo wa  kidigitali katika kuhifadhi nyaraka muhimu kwa faida ya vizazi vijavyo.

Akizungumza katika Semina hiyo Programu Afisa wa habari na Mawasiliano UNESCO, Lusajo  Mwaiteleke  amesema kuwa  Mwaiteleke ameeleza kuwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia wamejikita kuifundisha jamii namna ya kuitumia vyema kumbukumbu kwa njia za kidigitali ili kuweza kuondokana na changamoto zitakazojitokea katika uhifadhi wa taarifa zao.
 Mwasilishaji wa mada ambaye pia ni Mhifadhi kutoka Makumbusho ya Taifa bi.Flower Manase amewashauri viongozi wa vyombo vya habari kuweka mfumo imara wa kuhifadhi taarifa zao. Pia ameishauri jamii hasa serikali na taasisi binafsi kubadili namna ya kuhifadhi taarifa zao kila mara ili kukwepa usumbufu ikiwemo kupotea kwa taarifa zao za muhimu
“Napenda kuikumbusha jamii na wadau mbalimbali kutumia mikakati inayoendana na kasi ya mabadiliko ya mfumo huo hasa katika kuhifadhi taarifa muhimu katika vyombo vya kidijitali kwa lengo la kutunza kumbukumbu zao.”

Programu Afisa wa habari na Mawasiliano Tume ya Taifa UNESCO Lusajo Mwaiteleke akizungumza na waandishi wa habari.
Mhifadhi wa Makumbusho ya Taifa,  Dkt Amandus Kweka amesema athari hizo zinatokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki vinavyotumika kuhifadhi nyaraka hizo ikiwemo  kompyuta na simu. 
“Serikali inahamasisha jamii ihamie kwenye mfumo wa dijitali bila ya kuwa na mikakati ya kuhifadhi taarifa za nyuma...Inatakiwa tuwe na maandalizi ya namna gani tunatunza taarifa muhimu ili ziweze leta faida kwa vizazi vya baadae,” amesema na kuongeza.“Urithi wa kidijitali unaohifadhiwa kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo uko hatarini kupotea kutokana na kasi ya mabadiliko ya mfumo huo yanayotokea mara kwa mara yasiyoepukika,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here