Msajili wa Vitambulisho Dina Kaka akifafanua jambo leo jijini Dar es Salaam kuhusu utaratibu wa kupata vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Charles E. Kichere, akimkabidhi kitambulisho mfanyabiashara mdogo wa Soko la Kariakoo Bw. Mshamu Hassan.
Kitambulisho cha Mfanyabiashara mdogo
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles E. Kichere akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam kuhusu uzinduzi wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema.
WINGU
LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua utoaji wa Vitambulisho vya Wafanyabiashara
wadogo ambao wapo kwenye Sekta isiyo rasmi wakiwemo wamachinga.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam Kamishna Mkuu wa (TRA ) Charles
Kichere,
amesema kuwa utoaji wa vitambulisho hivyo kwa wafanyabiashara wadogo itasaidia kufanikisha ulipaji wa kodi.
Amesema
kuwa ili mfanyabiashara haweze kupata kitambulisho anatakiwa kujiunga
katika vikundi maalum vinavyotambulika kisheria na serikali.
Bw. Kichere
ameeleza mfanyabiashara huyo anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa, namba ya
utambulisho ya walipakodi ya kikundi alichojiunga pamoja na kuchangia Shillingi
10,000.
“Kitambulisho
hicho kitamsaidia mfanyabiashara kutambulika katika taasisi za fedha na
kupata mkopo ambao utakuwa msaada wa kukuza biashara yake” amesema Bw. Kichere.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema,
amesema kuwa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho ni mfanikio makubwa kwani mpango huo ulikuwa unasubiriwa zaidi ya miaka miwili.
Amesema
kuwa kufanikisha mpango wa vitambulisho sasa wamachinga watakuwa wanalipa kodi na kufanya kazi katika mazingira rafiki na kuwa tofauti na kipindi cha nyuma.
“Tutaendelea
kushirikiana na wamachinga ili wafanya biashara zao na kutambulika na serikali
bila kusumbuliwa na mtu yoyote” amesema Mhe. Mjema.
Utoaji
wa vitambulisho kwa wafanyabiashara unatokana na marekebisho ya sheria ya
usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 yaliofanyiwa marekebisho na kikao cha Bunge la
Bajeti mwaka wa fedha 2017/2018.
Miongoni
mwa marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum
wafanyabiashara wadogo ambao wapo katika sekta isiyokuwa rasmi.
Zoezi
la hilo linatekelezwa na TRA kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa
Usajili, Ufilisi na Udhamini (TIRA) pamoja na idara ya Uhamiaji.
TRA kwa
kushirikiana na wadau wengine ilianza kutekeleza jukumu hilo kwa kuutambua
Umoja wa Wamachinga wa Kariakoo jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kuwapatia
vitambulisho vya Taifa pamoja namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).
Hata
hivyo imeelezwa kuwa vitambulisho hivyo vya wafanyabiashara vitadumu kwa muda
wa miaka 3 ambapo vitakuwa na maelezo ya mfanyabiashara husika ikiwemo picha ya
mfanyabiashara, jina la eneo analofanyia biashara, namba ya utambulisho wa
mlipakodi na sahihi ya mfanyabiashara.
No comments:
Post a Comment