Mkurugenzi wa Utafiti wa Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka (WARAMI ) Phillipo Mwakibinga akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano na Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI Phillipo Mwakibinga jijini Dar es Salaam.
WINGU LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Watetezi wa
Rasilimali Wasio na Mipaka (WARAMI) wamewataka baadhi ya viongozi wa dini, siasa pamoja
na wanaharakati kuheshimu sheria za nchini ikiwemo kuto ingilia uhuru wa
mahakama kwa kutoa kauli za kushinikiza juu jambo fulani.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI
Phillipo Mwakibinga, amesema kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa
kiendesha vyama hivyo bila kufata misingi ya sheria.
Amesema kuwa
hivi karibu viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamekuwa wakitoa
kauli ya kushinikiza mahakama kwa kuwapa dhamana viongozi wao wa juu.
Mwakibinga amesema
kuwa viongozi wa siasa wamekuwa wakitoa kauli hiyo, huku wakijua mahakama ni
chombo cha haki ambacho akipaswi kuingiliwa na mtu yoyote kwa mujibu wa sheria.
“Kumekuwa na
kauli ambazo moja kwa moja zimelenga kuishawishi, kuishinikiza na kuilazimiisha
mahakama ifanye watakavyo wao kwa kuacha misingi ya haki wajibu na maadili ya
kimahakama”amesema Mwakibinga.
Ameeleza
kuwa watanzania wanapaswa kujua sheria ni kama ‘Kaa la moto’ na inapotokea mtu
umevunja sheriza lazima ujiandae kuungua.
Amesema kuwa
wakati umefika wa viongozi wa siasa kuacha kuongea maneno ambayo sio rafiki
katika jamii na kusababisha kuharibu sifa za vyombo vya kiusalama kwa kuongea
vitu vya ajabu.
Katika hatua
nyengine amewataka viongozi wa dini wakiwemo maaskofu’ wanaotumika na vyama vya
siasa kuacha tabia hiyo na badala yake kufanya kazi ya mungu.
Hata hivyo Mwakibinga
amesema kuwa WARAMI hawapo tayari kutoka katika msingi ya kuitetea jamii kwa
mslahi ya taifa.
No comments:
Post a Comment