KAMPUNI TATU ZAONGOZA MAUZO SOKO LA HISA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, January 16, 2018

KAMPUNI TATU ZAONGOZA MAUZO SOKO LA HISA

WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Meneja Mauzo Mwandamizi wa Soko la hisa Dar es Salaam Merry Kinabo
Mauzo ya hisa (Turnover/ Liquidity)
Mauzo kwa wiki iliyoishia 5 Januari 2018 yalikuwa shilingi bilioni 2.5 na wiki iliyoishia tarehe 11 Januari 2018 yakawa shilingi milioni 371.
  Idadi ya hisa zilizo uzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia tarehe 5 Januari 2018 zilikuwa hisa laki 8 na wiki iliyoishia tarehe 11 Januari 2018 idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa sokoni  ilikuwa hisa laki 7.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia tarehe 11 Jabuari 2018 ilikuwa kama ifuatavyo:
VODA……………………………………………76%
CRDB…………………………………………….11%
DSE……………………………………………….7.5%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko kwa umeshuka kwa Shilingi Bilioni 284 kutoka Shilingi Trilioni 23 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 22.7 wiki iliyoishia tarehe 11 Januari 2018. punguzo hilo limetokana na kushuka kwa bei za hisa za ACA (9%), NMG (8%), na EABL (2%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepanda kwa Shilingi Bilioni 2 kutoka Trilioni 10.285 hadi kafika Shilingi Trilioni 10.287 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa ya DSE (5%).
 Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeshuka kwa pointi 30 kutoka pointi 2,390 hadi 2,360 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Acacia (ACA), National Media Group (NMG) na East African Breweries Ltd (EABL).
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi 1 kutoka pointi 3,923 hadi pointi 3,924 kutokana na kupanda kwa bei za hisa za DSE.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 5,504.
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa poniti 2 kutoka pointi 2461 kadi pointi 2463.
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,462
Hati Fungani (Bonds)
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 11 Januari 2018 yalikuwa Shilingi bilioni 45 kutoka Shilingi 1.4 milioni wiki iliyopita ya 5 Januari 2018. 
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na nne (14) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 52.3 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 45.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here