OPERESHENI YA HESLB YALETA MATUMAINI ONGEZEKO LA WANUFAIKA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, January 17, 2018

OPERESHENI YA HESLB YALETA MATUMAINI ONGEZEKO LA WANUFAIKA

WINGU LA HABARI.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB) imewataka waajiri wa taasisi zote hapa nchini kupeleka marejesho ya asilimia 15 ya mishahara ya wanufaika wa mkopo wa elimu ya juu kwa wakati ili kuepuka adhabu inayoweza kutolewa. 


Akizungumza na waandishi wa habari katika Operesheni, Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji wa Mikopo Elimu ya juu Phidelis Joseph amesema ni vema kampuni na taasisi zote kupeleka marejesho hayo kwa wakati ili kuepuka migogoro.

Joseph ni mkuu wa opersheni, amesema kwa sasa bodi  inatembelea wateja wake wote kwa lengo la kutoa elimu pamoja na kuwakumbusha kulipa marejesho kwa wakati, kwani fedha hizo zinaitajika kwa ajili ya kusomesha wanafunzi wahitaji.


Akizungumza akiwa katika Kampuni ya Hegy Engineering, Joseph amesema kuwa endapo kampuni haitaweza kupeleka marejesho yao kwa wakati itachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.


Ameeleza kuwa ni vema kampuni kupeleka marejesho ya wanufaika kadri inavyowezekana pamoja na kutoa ushirikiano kwa bodi ya mkopo kwa kutoa taarifa za wafanyakazi ambao wameajiriwa.


"Baada ya mfanyakazi kuajiriwa, mwajiri anapaswa kuleta taarifa zake bodi ya mikopo ndani ya siku 28 baada ya kumujiri mtu mwenye elimu ya stashahada na shahada"amesema Joseph.


Amefafanu kuwa miongoni mwa taarifa ambazo mwajiri anapaswa kueta HESLB ni pamoja na jina la chuo, majina mwajiriwa ambayo alikuwa anatumia akiwa chuo, namba yake ya mthiani  (Index number).

Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji wa Mikopo Elimu ya juu Phidelis Joseph akiwa upande wa kushoto, katikati ni Msaidizi wa Mhasibu Anna Adolf Kampuni ya Sincro Sitewatch akifuatiwa na Afisa  Rasilimali watu katika kampuni hiyo. 
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kampuni Hegy Engineering, Benedic Mushi upande wa kushoto akiwa na  mwezake ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi Kawicho Ndeengeri .
Kwa upande wake,  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kampuni Hegy Engineering Benedict Mushi, amesema kuwa ndani ya mwezi huu watahakikisha walipa fedha zote wanazodaiwa na HESLB.

Amesema kuwa kuchelewa kuleta marejesho hayo imetokana na madeni mengi yanayosababishwa na hali ya kiuchumi kwa sasa.


“Tupo katika hatua ya mwisho kulipa gharama zote tunazodaiwa na serikali hivyo ndani ya mwezi huu tutalipa” amesema Mushi.

Hata  hivyo amesema  kuwa kila mtanzania anatakiwa kutoa ushirikiano ili kuchangia katika sekta ya elimu jambo ambalo linaweza kuleta maendeleo kwa taifa.




Mkurugenzi wa Ufundi Kawicho Ndeengeri amewataka waajiri kutoa ushirikiano kwa bodi ya mkopo jambo ambalo linaweza kusaidia kupatikana kwa fedha kwa ajili ya kusomesha wanafunzi waitaji.
Ndeenderi ameishauri HESLB kutafuta mbinu nyengine ya kutafuta wanufaika ambao wamejiajiri ambao kwa sasa wanafanya biashara.

Amesema wanufaika wengi wanafanya biashara ambapo bado hawajatambulika na bodi kwa ajili ya  kuanza kupeleka marejesho ya mikopo yao.

“Wanufaika wanapaswa kujitokea wenyewe na kuanza kulipa madeni yao, kwani kufanya hivyo itasaidia kuleta maendeleo kwa taifa” amesema Ndeenderi.
Katika Opresheni ambayo leo imeendelea, HESLB imefanikiwa kuwatembelea  Kampuni ya Hegy Engineering na Sincro Sitewatch ambapo zimepigwa faini (penati) ya milioni 9 baada ya kuchelewa kupeleka marejesho ya  asilimia 15 ya mishahara ya wanufaika. 

Hata hivyo wameonyesha ushirikiano wa kulipa fedha hizo kwa kadri inavyowezekana pamoja na kutoa ushirikiano kwa bodi ya mkopo kwa kutoa taarifa za wafanyakazi ambao wameajiriwa katika kampuni hizo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Urejeshaji wa Mikopo Elimu ya juu Phidelis Joseph akifafanua jambo wakati akizungumza na uongozi wa  Kampuni ya Hegy Engineering leo jijini Dar es Salaam.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa. jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here