Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji Manispaa ya
Kigamboni Dotto Msawa akifatiwa na Afisa Mipango Miji Manispaa ya Kigamboni Nice William
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni
Hashim Mgandilwa, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
WINGU
LA HABARI.
NA NOEL
RUKAUGA, DAR ES SALAAM
Wadau
mbalimbali nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika Wilaya ya
Kigamboni ambapo kuna asilimia 70 ya maeneo ambayo hayaendelezwa kwa ajili ya
shughuli za kiuchumi.
Akizugumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim
Mgandilwa, amesema kuwa kigamboni
bado kuna maeneo rafiki kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo viwanja vya ufukweni.
Amesema
kuwa tayari wametenga maeneo ya uwekezaji ikiwemo viwanda, kwani baada ya
kufanya operesheni imebainika bado kuna fursa ya asilimia 70 kwa ajili ya
shughuli za kiuchumi.
Mgandilwa
amewataka watu wote ambao wanamiliki maeneo ya ufukweni katika wilaya hiyo, kufanya
uwekezaji kama ilivyokusudiwa ili serikali iweze kukusanya kodi kwa ajili ya
ujenzi wa taifa.
“Kuna wakazi
wa kigamboni maeneo ya ufukweni wamefanya makazi badala ya kufanya
uwekezaji…natoa muda wa mwezi mmoja ili waweze kufanya uwekezaji, kama
wakishindwa tutapendekeza viwanja waviache” amesema Mgandilwa.
Ameeleza
kuna watu wengi wanaoyesha nia ya uwekezaji katika maeneo ya ufukweni, lakini
kuna baadhi wemekaa nayo maeneo hayo kwa muda mrefu ila kuyaendeleza.
“Serikali
inaitaji kodi, unapokaa eneo la uwekezaji bila kuliendeleza ni kuikosesha
mapato” amesema Mgandilwa.
Aidha
ameeleza kuwa wakazi wote wilaya ya kigamboni wanatakiwa kuomba vibali kabla ya
kujenga ili kuepuka kujenga katika maeneo ambayo sio rasmi.
Afisa
Mipango Miji Manispaa ya Kigamboni Nice William, amesema kuwa wataendelea kutoa
ushirikiano kwa kila mkazi wa wilaya hiyo hasa katika kujenga kwa kufata
taratibu.
“Tumejipanga
kuendeleza mji wa kigamboni ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira rafiki”
amesema William.
Mwenyekiti
wa kamati ya uwekezaji Manispaa ya Kigamboni Dotto Msawa, amesema kuwa wakati
umefika wawekezaji kuwekeza kigamboni kutokana kuna mazingira rafiki.
Amesema
kuwa mpaka sasa ni asilimia 30 ambayo imetumika katika uwekezaji katika wilaya
hiyo, huku akieleza kuwa wamejipanga kufaya maboresho ili kuhakikisha kuna kuwa
na vyazo vingi vya mapato.
No comments:
Post a Comment