CHUO CHA TAIFA UTALII YALETA FURSA SIKU TAMASHA APRIL27 MWAKA HUU. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, April 23, 2018

CHUO CHA TAIFA UTALII YALETA FURSA SIKU TAMASHA APRIL27 MWAKA HUU.

Picha ya Mussa Khalid
Watatu kutoka kushoto  ni Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Shughuli za Kitaalam katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Stephen Madenge akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam

WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kimeandaa tamasha la siku ya taaluma lenye ujumbe ‘fursa ya ajira kwa vijana kupitia taaluma ya ukarimu na Utalii’ linalotarajia kufanyika aprili 27 mwaka huu katika Kampasi ya Bustani jijini Dar es Salaam.
 Tamasha hilo limelenga kuendelea na kukuza ukuzaji wa sekta ya utalii na ajira nchini, kuwaleta pamoja wadau mbalimbali pamoja na kuhamasisha umma kuhusu mafunzo na huduma zitolewazo na chuo cha utalii.
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Shughuli za kitaalam katika chuo cha Taifa cha Utalii Stephen Madenge, amesema lengo ni kuhakikisha wanawaleta wadau mbalimbali karibu kupitia sekta ya utalii.
Magenge amesema sekta ya utalii nchini haijapungua kwani imeendelea kufanya vizuri kwa kuweza kupata watalii ukilinganisha na nchi zinazozunguka Afrika Mashariki, hivyo wataendelea kutoa elimu ya utalii kwa watanzania.
"Kwa kutumia tamasha hili wanafunzi wataonesha kwa vitendo uhodari wa taaluma zitolewazo chuoni ikiwa ni pamoja na Live Cooking,Cocktail na pastry product makini pamojana na wine testing and testing preparatioin” amesema Madenge.
 Amesema kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na uwasilishwaji wa mada za ukarimu na utalii kutoka kwa wataalamu mahiri wa sekta ya ukarimu na utalii wa hapa nchini.
 Madenge ameeleza kuwa kupitia tamasha hilo wanategemea kuwaunganisha na kuwaleta kwa pamoja wadau mbalimbali wa vyuo vya hotel, kampuni za kitalii, mawasiliano, banki, taasisi, idara na wizara mbalimbali pamoja na kutoka shule mbalimbali za sekondari.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Eunice Ulomi, amesema kuwa wataendelea kuwafundisha wanafunzi elimu ya utalii ikiwemo utamaduni ili kutangaza asili ya mtanzania jambo litakalosaidia kuwavutia watalii hapa nchini.
 Amesema kuwa wataendelea kuelimisha jamii katika sekta ya utalii na utamaduni kwa ujumla jambo ambalo litasaidia kuwaleta  pamoja na wadau mbalimbali.
“Chuo kinaendelea kutoa mafunzo katika taaluma ya utalii na ukalimu..kufanya hivyo tunaamini kutaendelea kukuza utalii na utamaduni hapa nchini” amesema Ulomi.
Mkuu wa Kampasi ya Temeke Martina Hagweti, amesema kuwa wanaendelea kuwahamasisha watanzania kuwa na dhana ya kujiwekea mazoea ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
 Hata hivyo ameeleza kuzingatia ukuaji wa sekta ya utalii na ajira hapa nchini chuo kitaendelea kutoa mafunzo bora kwa wanafunzi ili kuhakikisha kinaendelea kufanya vizuri.
 Katika tamasha ya siku ya taaluma linatarajiwa kufanyika April 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe. Generali Gaudence Milanzi.
Chuo cha Taifa cha Utalii  ni wakala uliopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo wana dhamana ya kutoa mafunzo ya ukarimu na utalii nchini pamoja kutoa ushauri wa kufanya tafiti.
 Chuo cha Taifa cha Utalii kinaithibati kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kutoa mafunzo ya ukarimu na utalii kwa ngazi ya Stashahada, Astashahada pamoja na mafunzo mafupi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here