BENKI YA DTB YATOA FURSA KWA WAFANYABIASHARA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, February 27, 2018

BENKI YA DTB YATOA FURSA KWA WAFANYABIASHARA

 Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji na Meneja Mkuu wa DTB Benki Viju Cherian pamoja akiwa Mkuu wa Bidhaa za Masoko benki ya DTB Sylvester Bahati wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu uzinduzi kampeni ya Chakarika II.
Mkuu wa Bidhaa za Masoko benki ya DTB Sylvester Bahati kizungumza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Benki ya DTB Tanzania (Diamond Trust Bank) imewataka wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa ya kupata mkopo hadi sh milioni 500 baada kufunua akaunti ya biashara kupitia kampeni ya Chakariki II ambayo inatoa nafasi kwa wateja kupata mkopo ndani ya siku tano baada ya kukidhi vigezo.

Chakarika ni kampeni ambayo imelenga kuwasaidia wafanyabishara wadogo na wakati katika katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kuwapunguzia gharama pamoja na kupata huduma kwa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi kampeni ya Chakarika, Mkurugenzi Mtendaji na Meneja Mkuu wa DTB Benki Viju Cherian amesema kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya biashara katika kuendeleza uchumi wa viwanda wameamua kuleta kampuni hiyo ili kufanikisha malengo ya Serikali.

Amesema kuwa benki ya DTB imedhamiria kutekeleza uboreshaji wa akaunti za biashara ili kuwasaidia wafanyabiasha pamoja na kuwa na warsha kwa wafanyabiasha wadogo wapate elimu katika kufanisha mipango yao ya kibiashara.

Cherian amesema kuwa akaunti ya biashara ya DTB inapatikana kwa Sh 50,000 na makato yake ya mwezi yakiwa sh 12,000, ambapo wateja watakao fungua kipindi hiki cha kampeni ya Chakarika wataweza kujishindia zawadi mbalimbali pamoja na kupata mialiko ya kuhudhuria warsha za biashara zinazoendelea.

Kwa upande wake Mkuu wa Bidhaa za Masoko benki ya DTB Sylvester Bahati, amesema kuwa mkopo hiyo itatolewa kwa wateja ambao wamezewa kukidhi vigezo.

Bahati ameeleza kuwa wafanyabiasha wakubwa watafungua akaunti kwa sh 100,000 huku wafanyabiasha wadogo watapata fursa ya kufungua akaunti hiyo kwa sh 50,000.

“Tumeamua kufanya hivyo ili kuwapa nafasi wafanyabiasha wadogo waliopo katika mji midogo waweze kufungua akaunti katika benki yetu DTB ili waweze kunufaika na huduma zetu” amesema Bahati.

Katika hatua nyengine Bahati amefafanua kuwa benki ya DTB kwa sasa ina matawi 28 hapa nchini,  ambapo matawi 14 yapo katika jiji  la Dar es Salaam huku matawi mengine yakiwa katika mkoa wa Mwanza, Arusha, Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Tabora, Tanga pamoja naVisiwa vya Zanzibar.

Benki ya DTB Tanzania ni Kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) yanayoendesha shughuli za kibiashara katika  ukanda wa Afrika Mashariki nchini Kenya, Uganda pamoja na Burundi.

Pia ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya kiuchumi (The Aga Khan Found for Economic Development-AKFED) ambayo ni tawi la mtandao wa maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network -AKDN)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here