Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi Taifa (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Serikali imetakiwa kupanga bajeti inayotekelezeka ili
kufanikisha utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo zinazokusudiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati
akitoa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, Mwenyekiti wa
Chama Cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa serikali inapaswa
kupanga bajeti kulingana na matumizi halisi.
Prof. Lipumba amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Benki
Kuu ya Tanzania katika kipindi cha miezi saba kunzia julai mwaka wa jana hadi
januari mwaka huu, serikali ilipanga kutumia shilling trilioni 15.5 lakini
matumizi halisi yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 10.7.
Amesema kuwa matumizi hayo ni sawa na asilimia 69 ya bajeti
hiyo ambayo utekelezaji wake unasuasua kwa katika kipindi hicho serikali
ilitenga shilingi trilioni 7.4 kwa ajili ya kutumia kwenye miradi ya
kimaendeleo.
“Ni vema bajeti zetu zikawa zinazingatia hali halisi
kutokana kumekuwa na matumizi madogo kuliko bajeti” amesema Prof. Lipumba.
Prof. Lipumba ambaye ni mchumi anafafanua kuwu makadirio ya
ukusanyaji wa kodi ni mkubwa kuliko ukusanyaji halisi kwani mwezi julai mwaka jana
hadi januari mwaka huu mapato yote ya serikali yalikadiriwa kuwa shilingi
trilioni 11.7 lakini makusanyo ni trilioni 10.2 ambapo sawa na asilimia 88.
Amesema kumekuwa na mzunguko mdogo wa fedha (Currency in
circulation) kutoka shilingi trlioni 3.8 kwa mwezi oktoba 2015 na kufikia
shilingi trilioni 3.4 april mwaka wa jana, jambo ambalo sio rafiki kwa uchumi
wa nchi.
Hata hivyo mchumi huyo ameipongeza serikali kwa juhudi za
kukusanya mapato na kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo kujenga reli ya kisasa
pamoja na kufua umeme wa maji kwenye maporomoko.
No comments:
Post a Comment