Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa DSE, Mary Kinabo.
WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity).
Mauzo kwa wiki iliyoishia 9 March 2018 yalikuwa shilingi Milioni 518 ikilinganishwa na mauzo ya shilingi bilioni 2.9 kwa wiki iliyoishia tarehe 2 Machi 2018.
Vile vile Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia tarehe 9 March 2018 ni hisa laki 6.9 ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya milioni 2.4 kwa wiki iliyoishia tarehe 2 Machi 2018.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia tarehe 9 March 2018 ilikuwa kama ifuatavyo:
VODA……………………………………………51%
TBL …………………………………………….18%
DSE………………………………………………11%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa Shilingi Bilioni 417 kutoka Shilingi Trilioni 23.1 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 22.7 wiki iliyoishia tarehe 9 Machi 2018. Ongezeko hilo limetokana na kushuka kwa bei za hisa za NMG (8%), KCB (7%) na ACA (5%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani kwa wiki imeishia 9 Machi 2018 ni shilingi Trilioni 10.2 kama ya wiki iliyoishia 2 Machi 2018.
Viashiria (Indices).
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepungua kwa pointi 43 kutoka pointi 2,405 hadi 2,362 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za National Media Group (NMG), Kenya Commercial Bank (KCB) Acacia Mining (ACA)
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 3893.
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 5365 kama wiki iliyopita
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 2574 kama wiki iliyopita
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kwenye wastani wa pointi 2463 kama wiki iliyopita
Hati Fungani (Bonds).
Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 9 Machi 2018 yalikuwa Shilingi bilioni 65 kutoka Shilingi Bilioni 4 wiki iliyopita ya 2 Machi 2018.
Mauzo haya yalitokana na hatifungani kumi na mbili (12) za serikali zenye jumla ya thamani ya Shilingi bilioni 69 kwa jumla ya gharama ya Shilingi bilioni 65
No comments:
Post a Comment