Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo (aliyesimama mbele) akiwaelimisha baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina Maalum iliyohusu masuala ya kodi hususani katika matumizi ya mashine za Kielektriniki za kutolea Risiti (EFD), masuala ya utoaji taarifa ya fedha mpakani pamoja na masuala ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayotarajiwa kuanza mapema tarehe 5 - 9 Machi mwaka huu.
Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) , Bibi Diana Masalla (aliyesimama mbele) akiwaelimisha baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina Maalum iliyohusu masuala ya kodi hususani katika matumizi ya mashine za Kielektriniki za kutolea Risiti (EFD), masuala ya utoaji taarifa ya fedha mpakani pamoja na masuala ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi inayotarajiwa kuanza mapema tarehe 5 - 9 Machi, mwaka huu.
Baadhi ya Waandishi wa habari waliohudhuria Semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada toka kwa baadhi ya Watendaji wa Mamlaka hiyo (hawapo pichani) katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
WINGU
LA HABARI.
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imesema itaendelea kuwapa ushirikiano waandishi wa
habari kwa kuwajengea uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya kodi ili kuhakikisha
wanaelimisha umma kwa kutoa taarifa sahii.
Akizungumza
katika semina iliyoandaliwa na TRA kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wahabri ,
Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa mlipa kodi TRA, Richard Kayombo amesema kuwa waandishi
wana mchango mkubwa katika kuibalisha umma.
Amesema
kuwa katika waandishi wa habari, bloger ni kundi kubwa ambalo limekuwa na mchango katika jamii katika
kufikisha habari kwa haraka kuliko vyombo vingine vya habari.
“Tumeanua
kuwapa semina watu wa bloger kutokana wao wanatusaidia kutoa taarifa zetu sahii
na kwa wakati, hivyo tumeona tuwapa elimu ya kodi ili waweze kutusaidia
kuelimisha umma juu ya umuhimu wa ulipaji wa kodi” amesema Kayombo.
Hata
hivyo amewataka bloger wawe katika vikundi na kujisajili ili waweze kufanya
kazi na makapuni au taasisi mbalimbali na kuingia katika malipo rasmi.
“Bloger
waweze kujisajili kikundi au mmoja mmoja na kufanya biashara yao kuwa rasmi
ambapo watapa TIN namba na reseni ya biashara na kupata fursa ya kufanya kazi
na kampuni au taasisi na kuweza kulipwa katika njia rasmi” amesema Kayombo.
Amefafanua
kuwa katika semina hiyo wamesisitisha katika maeneo ambayo ni mpya hasa katika
ulipaji wa kodi majengo ambayo inalipwa mara moja kwa mwaka.
“Tumewafundisha
utaratibu mpya wa kulipa kodi ya majengo kwa kutumia simu za mkononi na tovuti
ambayo inaweza kuondoa usumbufu” amesema Kayombo.
Kayombo
ameeleza kuwa wateja wanapaswa kuwa mwamko wa kuomba risiti pamoja na kukagua risiti
kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kutokuwa waminifu kwa kutoa risiti feki.
Kwa
upande wa bloger wameishukuru TRA kwa kuwapatia semina hiyo ambayo imewasaidia
kuwaongezea uwelewa wa masaula mbalimbali ya kodi.
No comments:
Post a Comment