Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Likokona Mkoani Mtwara akipokea kitabu kutoka kwa Afisa wa Elimu Sekondari Wilaya ya Nanyumbu Bw. Luoga Musijack
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Likokona akirusha mpira juu baada ya shule yake kupokea msaada wa vifaa vya michezo pamoja vitabu vya masomo mbalimbali ya sekondari kutoka Kampuni ya Watumish Housing (WHC).
Baadhi ya vitabu vilivyotolewa na WHC katika Shule ya Sekondari Likokona.
Kutoka kushoto ni Afisa wa Elimu Sekondari Wilaya ya Nanyumbu Luoga Musijack pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule Kikokona Eugen Ludovick wakishika mpira baada ya kupokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka WHC.
Kutoka kushoto ni MKurugenzi Mtendaji wa WHC, Dk. Fred Msemwa akimkabidhi vitabu vya masomo mbalimbali ya sekondari Afisa wa Elimu Sekondari Wilaya ya Nanyumbu Luoga Musijack.
WINGU LA HABARI
NA
MWAANDISHI WETU, MTWARA.
Kampuni
ya Watumishi Housing (WHC) imetoa msaada wa vifaa vya michezo pamoja na vitabu mbalimbali
vya kujifunzia katika shule ya Sekondari Likokona iliyopo Wilaya ya Nanyumbu
Msasi Mkoani Mtwara.
WHC ni
wajenzi ambapo wametoa msaada huo kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu katika
kuhakikisha shule zenye mazigira magumu kufikika wanapata huduma mbalimbali pamoja
na kupeleka miradi ya nyumba za walimu kwa kushirikiana Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA).
Akizungumza
baada ya kupokea msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo mipira ya miguu pamoja
vitabu vya masomo mbalimbali ya sekondari kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa WHC
Dk. Fred Msemwa, Afisa wa Elimu Sekondari Wilaya ya Nanyumbu Luoga Musijack,
amesema kuwa ameishukuru WHC kwa msaada huo ambapo anaamini itakuwa chachu ya
kufanya vizuri kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule Kikokona Eugen Ludovick, amesema kuwa vifaa vya
michezo na vitabu vitawasaidia wanafunzi kujifunza kupitia masomo yao.
“Ni
hatua nzuri ambayo WHC wameonyesha kwa kutoa msaada wa vitabu na vifaa vya
michezo ambapo tumepokea kwa mikono miwili na uogonzi wa shule pamoja na wanafunzi
kwa ujumla” amesema Ludovick.
Shule
ya Sekondari Likokona ni moja wopo kati ya shule za kata zilizonufaika na mradi
wa ujenzi wa nyumba za walimu katika maeneo magumu kufikika hapa nchini, ambapo
mradi huo unatekelezwa na WHC kama wajenzi kwa kushirikiana TEA ambao wafadhili
wa mradi huo.
Ujenzi
wa nyumba hizo za walimu zimekamilika na nyumba zimeshakabidhiwa kwa walimu na
kuanza kuishi ili wafanye kazi katika mazingira rafiki.
WHC ni wajenzi ambapo wamekuwa wakitekeleza miradi
mbalimbali ya ujenzi kwa gharama nafuu tofauti na kampuni nyingine zinazofanya
kazi ya aina hiyo.
Hata
hivyo wamepewa jukumu na serikali kujenga nyumba za watumishi wa umma na
kuwakopesha kwa mikopo nafuu na ya muda mrefu kwa watumishi wote wanaishi ndani
na nje ya nchi na sasa wapo katika awamu ya kwanza ya kutekeleza maagizo hayo.
WHC
inafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na
Mashirika yote ya Pensheni ikiwemo Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa
Serikali(GEPF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii(NSSF), Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF), Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma(PPF), pamoja
na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
No comments:
Post a Comment