Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Rehema Ludanga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu Kongamano siku ya wanawake.
WINGU LA HABARI
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) imeandaa kongamano la siku ya wanawake linalotarajia kufanyika machi 7 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Rehema Ludaga amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kufanya tathmini kuhusu masula mbalimbali yanayotokea kwa wanawake katika maeneo yao ya kazi.
Ludanga amesema katika kongamano hilo watajadili mada mbalimbali yenye lengo la kutatua changamoto za wanawaze na kuleta usawa kutokana wakinamama ni kundi maalumu ambapo TUCTA kupitia vyama shiriki wataendelea kusimama kidete kuwatetea.
"Kongamano hili tutajadili nafasi ya mwanamke katika mahala pa kazi na kuona changamoto gani wanakutana wanawake wakiwa sehemu za kazi...kuelekea siku ya wanawake duniani inafanyika kila machi 8 mwaka huu" Ludanga
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TUCTA, Dk. Yahya Msigwa amesema kila mwaka wanafanya kongamano ila kuweza kupata mawazo ya wanawake ili waweze kufanya maboresha ya sehemu zao za kazi.
Katika kongamano hilo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema, huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Tathimini ya Unyanyasaji wa kijinsia mahala sehemu ya kazi.
No comments:
Post a Comment