Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) Boniface Chandaruba akiwaonyesha waandishi wa habari fomu maalum ya usajili leo jijini Dar es Salaam.
WINGU
LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Serikali
imeawataka watanzania wenye taaluma na ujuzi katika sekta ya Mafuta na Gesi kuchangamkia
fursa za ajira zaidi ya 1,000 zinazotokana na mradi wa bomba la mafuta.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa
Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) Boniface Chandaruba, amesema kuwa watanzania
wote wenye sifa wanapaswa kujisajili TaESA ili waweze kuingizwa kwenye
kanzidata ya wakala.
Amesema
kuwa kufanya hivyo itasaidia serikali kubaini idadi halisi ya watanzania walio
na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi wa bomba la
mafuta.
“Zoezi
hili la usajili linafanyika bure hivyo, tunasisitiza kuwa hakuna gharama yoyote
itakayotozwa kwa mtanzania yeyote atakayehitaji kusajiliwa” amesema Chandaruba.
Chandaruba
amefafanua kuwa zoezi la usajili linafanyika kwa kujaza fomu maalum
inayopatikana kupitia tovuti ya wakala www.taesa.go.tz
au muhusika anaweza kufika katika ofisi za kanda zilizopo Mkoa wa Dar es
Salaam, Arusha, Dodoma pamoja na Mwanza.
Mradi
wa ujenzi wa bomba la mafuta la kusafirisha mafuta Ghafi ‘East Africa Crude Oil
Pipeline’ (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Changoleani mkoani Tanga
nchini Tanzania.
Mradi wa
bomba la mafuta ni mradi mkubwa kutekelezwa hapa nchini ambao unategemea kugharimu
dola za kimarekani bilioni 3.5 ambapo sawa na trillion 8 zitanzania.
Bomba
hilo linategemea kuwa na urefu wa kilometa 1,445, huku ujenzi wa kilometa 1, 115 za bomba hilo
utafanyika nchini ambapo jumla ya Mikoa
8, Wilaya 24, Vijiji 184 hapa nchini vinategemea kupitiwa na bomba hilo.
Mradi
wa ujezi huo unatarajia kuchukua kati ya miezi 24 hadi 36 hadi kumalizika
ambapo unatarajia kuzalisha fursa za ajira takribani 10,000 wakati wa ujenzi na
ajira zaidi ya 1,000 wakati wa uendeshaji wake.
No comments:
Post a Comment