WINGU
LA HABARI
HUSSEIN
NDUBIKILE NA ISAAC MAGESA, DAR ES SALAAM.
KAMPUNI
ya Usambazaji wa Mbolea ya Yara Tanzania Ltd imetangaza punguzo la bei ya mbolea
ya YaraMila Otesha kwa asilimia 50 huku ikibainisha lengo lake ni kuwawezesha
wakulima kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza
na wanahabari leo jijijni Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni hiyo nchini
Linda Byaba, amesema punguzo hilo litawasaidia wakulima kumudu gharama za mbolea
itakayowazesha kupata mavuno mengi ukilinganisha na mbolea nyingine ambazo
hazina ubora unaotakiwa.
“
Mbolea hii tuliizindua mwaka jana ina virutubisho saba ,sifa ya kuyeyuka haraka kwenye udongo, uwezo wa kufanya kazi
ndani ya siku mbili hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao pamoja kutochachusha udongo,” amesema.
Byaba
amesema mbolea hiyo ina ubora wa kupandia mazao ya aina zote ikiwemo Mahindi,
Chai,Sukari, Alizeti,Tumbaku, Mpunga, Viaz na Mbogambogai huku akibainisha
asilimia 50 ya wakulima waliokwishaitumia imewaongezea uzalishaji wa mazao.
Amebainisha
kuwa mbolea ya YaraMila Otesha ina virurubisho saba na kwamba kila punje moja ya
mbolea hiyo ina virutubisho vyote vikiwemo Nitrojeni, Fosiforasi, Kalsim ,
Boroni na Magneziam.
Amefafanua
kuwa mbolea hiyo inapatikana dunia nzima huku akitilia mkazo wakaulima wa
mbogamboga na nafaka katika nchi ya Tanzania, Rwanda na Burundi wanafafaidika
nayo.
Aidha,
amesema sifa nyingine za mbolea hiyo ni kuchochea machipukizi mengi yanayoleta
mavuno mengi katika zao la mpunga, utoaji mizizi mingi, hivyo kuufanya mmea
kuwa imara muda wote pamoja na kuwa na kiwango cha juu kirutubisho cha
Fosforasi ukilinganisha na mbolea nyingine za kupandia.
Ameawashauri
wakulima kuachana na mbolea zilizopitwa na wakati na zizizo na virutubisho
sahihi kwani mbolea ya kampuni hiyo hutoa majibu haraka.
Ameeleza
kuwa mbolea hiyo husambazwa kupitia usafiri wa reli, mawakala wakubwa wa mbolea
kwa kutumia usafirishaji wa malori.
No comments:
Post a Comment