Kutoka kushoto ni Meneja wa Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar Bw. Nicolas Cedro akiwa na Meneja wa Masoko na Mawasiliano Bi.Milvas Burnice.
WINGU LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Hoteli ya Park Hyatt
Zanzibar imemtambulisha Nicolas Cedro kama meneja mpya atakayeendesha hoteli
hiyo yenye hadhi ya nyota tano iliyopo katika eneo maarufu la kisiwani humo
linalojulikana kama Stone Town.
Cedro ambaye analeta
uzoefu mkubwa kutoka katika sekta ya hoteli amefanya kazi katika hoteli zenye
chapa maarufu duniani kama Hyatt, Melia pamoja na La Manga and Marriott.
Hata hivyo ni mwanachama
wa shirikisho la kimataifa la wahusika wa masuala ya vyakula kinachojulikana
kwa kifaransa kama “La Confrerie de la Chaine des Rotisseurs.”
Cedro ambaye ana Shahada
mbili za masuala ya vyakula na uendeshaji hoteli kutoka chuo kikuu cha hoteli
kilichopo Nice nchini Ufaransa pia ana Shahada ya uzamili ya uendeshaji wa
hoteli kutoka katika chuo kikuu cha E Cornel.
Cedro alianza kazi kama
mpishi akiwa nchini Hispania na toka wakati huo ameshafanya kazi katika nchi
mbalimbali duniani zikiwemo Hispania, Ufaransa, Qatar, Yordani na Tanzania bara
katika hoteli ya Hyatt Regency kama Mkurugenzi wa Chakula na Vinywaji.
Meneja huyo anasifika
kwa uadilifu wake katika uongozi na kuhamasiha ubora katika kazi na pia
anazungumza lugha za kifaransa, kiingereza na kihispania.
Katika kipindi cha miaka
25 ambacho amekuwa akifanya kazi amewahi kupata tuzo mbalimbali za ubora za
kimataifa na pia amewahi kupika kwa ajili ya watu maarufu wakiwemo Rais wa
zamani wa Ufaranza Jacques Chirac na Mfalme wa Malaysia.
Uzoefu wa Cedro, elimu,
ujuzi wa lugha pamoja na ubunifu ni vitu muhimu ambavyo meneja huyo atatumia
katika kujenga sifa na ubora wa hoteli hiyo na pia kwa wafanyakazi wake.
Akiwa kama Meneja wa
hoteli ya Park Hyatt Zanzibar na Cedro na timu yake kwa pamoja wana lengo kuu
la kuipandisha hoteli hiyo kuwa katika viwango vya juu zaidi na hivyo kuchangia
katika juhudi za taifa za kuhamasisha utalii nchini ikiwemo kisiwani humo.
“Napenda kufanya kazi
katika bara la Afrika na hasa katika kisiwa cha Zanzibar. Ni mahali ambapo kuna
mazingira mazuri na watu wenye upendo. Nimeshafanya kazi Tanzania kwa zaidi ya
miaka mitatu sasa katika hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro, Melia Zanzibar
na sasa hapa Park Hyatt Zanzibar. Nimesikia furaha kubwa sana kupata nafasi hii
ya kuendesha hoteli hii na nategemea kutumia ujuzi na uzoefu wangu ili kuleta
ladha ya kipekee katika chakula na pia huduma tutakazowapatia wateja wetu,”
alisema Cedro.
Cedro ambaye alianza
kazi ya upishi akiwa kijana wa miaka 17 anatambua umuhimu wa kuibua na kulea
vipaji vya vijana na hivyo anategemea kushiriki katika shughuli za kijamii
akiwa Zanzibar kwa kushirikiana na shule mbalimbali za kisiwani hapo za mapishi
ili kusaidia vijana wenye vipaji vya upishi waweze kupata ujuzi wa kimataifa
alio nao na hivyo waweze kujiendeleza katika fani hiyo na kuitumia kama njia ya
kujiinua kiuchumi.
Hoteli ya Park Hyatt
Zanzibar ni Hoteli ya kipekee na yenye historia ndefu hasa kwa kuwa katika eneo
maalum lililotengwa kama urithi na shirika la kimataifa la UNESCO.
Hoteli hiyo inatumia
jengo ambalo lililojengwa katika miaka ya 1847 hadi 1850 na aliyekuwa rafiki wa
mtawala wa wakati huo Sheikh Seyyid Said.
Jengo hilo linalojulikana
kama ‘Mambo Msiige’ ni mfano mzuri wa majengo ya kitamaduni ya Zanzibar likiwa
na mandhari ya kiarabu na linasadikika kuwa ni imara kutokana na udongo wake
uliotumika kujenga uliokuwa umechanganywa na maelfu ya mayai.
Hoteli hiyo
iliyosheherekea miaka mitatu toka kuanzishwa kwake tarehe 8 Machi mwaka huu,
imejijengea umaarufu mkubwa kwa kipindi kifupi kimataifa na nchini na
inashiriki ipasavyo katika kutangaza kisiwa cha Zanzibar kama moja ya maeneo ya
kipekee kwa utalii.
Kuhsu Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar.
Park
Hyatt Zanzibar inapatikana katika fukwe iliyoko katika mji kongwe wa Stone Town
na kituo cha urithi wa kimataifa yaani “UNESCO Heritage site”.
Hoteli
hiyo iko katika jengo maarufu lijulikanalo kama ‘Mambo Msiige’ lililo na
historia ndefu yenye izizi yake toka karne ya 17.
Eneo
la makazi la Zamani liko pembeni mwa jengo la Mambo Msiige na linatoa huduma ya
kipekee ya maakuli yenye eneo la kupumzika, maktaba na mkahawa wenye baraza
inayotazama fukwe ikiwa ni mandhari ya kipekee na kutoa huduma za chakula
kutoka kwa malighafi za kisiwani hapo.
Hoteli
inatoa huduma ya vyumba 67 vya kifahari vya kulala wageni vilivyomo katika
majengo hayo mawili, vyakula vyenye ladha ya kiasilia na pia bwawa la kuogelea
la kipekee kabisa linalounganika na bahari na pia sehemu ya kufanyia mazoezi.
Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar inakaribisha
wageni mbali mbali wakiwemo watalii, wafanya biashara na wasafiri wengine
wanaopendelea huduma za kipekee na kimataifa.
Chapa ya Park Hyatt inasifika kwa kutoa huduma kwa wafanya biashara na
wageni wanaotaka starehe kwa kuwapatia huduma wateja wake kwenye mandhari
mazuri wakiwemo sehemu za malazi na pia huduma binafsi za kipekee katika
mazingira faragha.
Zikipatikana katika maeneo mbalimbali maarufu duniani kila hoteli ya Park
Hyatt imeundwa katika mtindo wa kisasa wenye mandhari ya eneo ilipo.
Hoteli za Park Hyatt zina vyumba vya kulala wageni, vyumba vya mikutano
na maeneo ya matukio maalumu kwa vikundi mbalimbali na imepata sifa nyingi za
kimataifa kwa kazi za kisanii, chakula na vinywaji na pia kwa kuwa na wapishi
wenye sifa na kutunikiwa tuzo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment