Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dk. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Maadhimisho ya wiki ya elimu juu ya ugonjwa wa Shinikizo la Macho ambapo huadhimishwa duniani kote.
WINGU
LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Zaidi
ya watu milioni 253 duniani wanakadiliwa kuwa na matatizo ya kutokuona vizur, huku
idadi kubwa ya watu hawajui kama wanaugonjwa huo kutokana na kutokuwa na
utamaduni wa kuchunguza afya ya macho kama inavyoshauri na wataalamu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaaam, Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dk. Faustine Ndugulile, amesema kuwa kuna
idadi ya watu milioni 36 hawaoni kabisa.
Amesema
kuwa asilimia 2.8 ya watu wote wenye upungufu wa kutokuona vizuri ni sawa milioni
7 ambapo kati yao milioni 4.5 hawaoni kabisa.
“Zaidi
ya asilimia 75 ya visababishi vya kutokuona vizuri vinaweza kuzuilika au
kutibika” amesema Dk. Ndugulile.
Mwezi
march 11 hadi 17 mwaka huu ni wiki ya elimu ya ugonjwa wa shinikizo la macho
ambapo huadhimishwa duniani kote ikiwa ni mpango wa ulianzishwa na Chama cha
Wataalamu wa Afya.
No comments:
Post a Comment