Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza na mfanyabiashara katika ziara Mkaoni Katavi.
WINGU LA HABARI
Na Rachel Mkundai,
Katavi
Wafanyabiashara na
mkoa wa Katavi wamefarijika na ujio wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere katika mkoa wao na kusema kuwa
ziara hiyo imewasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kulipa kodi likiwemo
suala la usumbufu toka kwa mawakala wa kuuza na kusambaza mashine za EFD
kutokuwaletea mashine zao kwa wakati licha ya kuwa wamelipia takribani zaidi ya
mwaka mmoja.
Wafanyabiashara hao
wameyasema hayo mara baada ya kuzungumza na Kamishna Mkuu wa TRA
alipokutana nao katika ukumbi wa idara ya maji mjini Mpanda katika mwendelezo
wa ziara yake ya kuhamasiha wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki za
kutolea risiti EFD katika mikoa ya nyanda juu kusini pamoja na ile ya Magharibi
mwa nchi.
Wafanyabiashara hao
hawakusita kutoa shukrani zao kwa kusema kwamba ziara ya Kamishna Mkuu wa TRA
imekuja wakati muafaka kwa kuwa walikuwa na changamoto ambazo kwa muda mrefu
ziliwafanya wasilipe kodi na kupitia mkutano huo wamepata fursa ya kumweleza na
zimepatiwa ufumbuzi mara moja na zingine zilizobaki wana imani kuwa zitatatumliwa
kwa wakati na sasa wapo tayari kulipa kodi stahiki.
Mmoja wa
wafanyabiashara hao, akizungumza mara baada ya kurudishiwa pesa na wakala wa
EFD ambaye hakumpatia mashine yake kwa takribani miaka miwili, Bw. Kobra Kipara
amesema awali alitapeliwa pesa na wakala wa mashine za EFD lakini Kamishna Mkuu
amemtafuta wakala huyo na sasa amerudishiwa pesa zake.
Naye wakala wa uuzaji
na usambazaji wa mashine za EFD wa kampuni ya Pegamon Bw.David Nyaga ameahidi
kushirikiana na TRA kwa kuwasambazia wateja wake mashine za EFD kwa wakati na
kuweka mikakati ya kuwafikia wateja wao katika mikoa yote kwa kufungua matawi
ya ofisi zao na vile vile kutoa mafunzo ya namna ya kutumia mashine za EFD na kufanya
matengenezo kwa wakati.
Hata hivyo Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere ametoa wito kwa
wafanyabiashara kote nchini kutembelea ofisi za TRA ili kupata tafsiri sahihi
ya sheria za kodi na siyo kulipishwa kodi bila kuelewa.
Kamishna Kichere pia
amewaagiza maofisa elimu kwa mlipakodi wa TRA katika mikoa yote kuwafuata
walipakodi popote walipo na kuwapa elimu na tafsiri ya sheria za kodi ili
kuongeza uelewa wa masuala ya kodi miongoni mwa wafanyabiashara na jamii kwa
ujumla.
“Kama una shida, ni
vema ukaenda kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato, pamoja na kwamba tunatoa
elimu,lakini kama una shida, nenda ofisi ya TRA”, amesisitiza.
Bw. Kichere amesema
kodi zinatozwa kwa mujibu wa sheria, sasa kunaweza kuwa na tafsiri ndogo ya
kisheria au huelewi kitu, ametoa wito kwa wafanyabiashara kutembelea ofisi ya
TRA ili kuapata uelewa mzuri wa kodi na siyo kulipa tu kodi ambazo hawazielewi.
No comments:
Post a Comment