Waandishi wa habari wakiwa katika Mkutano na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere leo Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu sakata la Askofu Zachary Kakobe Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship kufuatia kauli yake kuwa “Yeye ana pesa kuliko Serikali" kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi Richard Kayombo.
WINGU
LA HABARI
NA NOEL
RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Taasisi
za dini nchini zimetakiwa kufata katiba zao pamoja na kulipa kodi stahiki kwa
wakati kupitia shughuli za kiuchumi wanazofanya ili kuepuka kuvunja sheria, kanuni na taratibu za kodi.
Hayo
yamesema leo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato (TRA) Charles Kichere, wakati akitoa taarifa ya uchunguzi kuhusu kauli
ya Askofu Zachary Kakobe ambapo alisema ‘Yeye ana pesa kuliko Serikali’.
Kamishna Kichele amesema kuwa Askofu
Kakobe hana akaunti katika taasisi yoyote ya fedha hapa nchini, huku akieleza
kuwa kanisa hilo limekuwa likikwepa kulipa kodi kutokana fedha walizowekeza
katika makapuni ya kukuza mitaji.
Amesema baada ya uchunguzi huo kanisa lilipa kiasi cha kodi cha sh
milioni 20,834,843 ambazo zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza
mitaji.
“Taasisi za dini zote ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi
zinapaswa kulipa kodi stahiki na kwa wakati na kufata sheria ili kuepuka usumbufu” amesema Kichere.
Ameeleza kuwa Kampuni inayomilikiwa na watoto wa Askofu Zachary
Kakobe pia ilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 37,280,030.00 ambazo nazo zimelipwa
baada ya uchunguzi.
Amefafanua kuwa baada ya uchunguzi huo Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
imebaini mambo kadhaa kutokana na kufanyika kwa uchunguzi huo.
Amesema kuwa uchunguzi
ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa
(Signatories) zilizopo katika benki ya NBC zenye jumla ya kiasi cha shilingi
8,132,100,819.00, amapo kiasi hicho cha fedha kimetokana na sadaka, zaka na changizo
ambazo zinatolewa na waumini wa kanisa hilo.
Kamishna Kichere
amesema Kanisa hilo linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na
‘majaba’ ambapo ni kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha, lakini uwekaji na utoaji
wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa
ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika.
Amesema kuwa kanisa halitengenezi hesabu za Mapato na Matumizi ya fedha kitu ambacho ni
kinyume na katiba ya kanisa pamoja na sheria za usimamizi wa fedha.
"Natoa wito kwa taasisi zote za dini ambazo zinajihusisha na shughuli yoyote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi" amesema Kamishna Kichere.
"Natoa wito kwa taasisi zote za dini ambazo zinajihusisha na shughuli yoyote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi" amesema Kamishna Kichere.
Katika hatua nyengine Kamishna Kichere amebainisha
kuwa Askofu Kakobe januari 24 mwaka huu, aliandika barua kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na kuomba radhi kutokana na kauli
yake ya kebehi pamoja na matamshi yake ya dharau kwamba ana pesa nyingi kuliko
Serikali.
Askofu Zachary Kakobe wakati akiendesha ibada katika Kanisa la
Full Gospel Bible Fellowship katika mahubiri aliyotoa kwenye Ibada
hiyo akisema “Yeye ana pesa kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania”.
No comments:
Post a Comment