WINGU LA HABARI.
NA MWANDISHI WETU.
Wekundu wa Msimbazi Simba Sport Clabu imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Gendarmerie ya Djibout katika mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika uliochezwa nchini Djibout leo.
Goli la Simba limefungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi dakika ya 55 kipindi chapili. Na kwa matokeo hayo wekundu hao wa Msimbazi wanasonga hatua ya pili ya mashindano kwa jumla ya magoli 5-0.
Itakumbukwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ilishindwa magoli 4-0 yalifungwa na John Bocco aliyefunga mawili, Emmanuel Okwi moja na Said Ndemla moja.
Hivyo katika hatua inayofuata Simba itakutana na klabu ya Al-Masry ya nchini Misri
No comments:
Post a Comment