Wakuu wa Wilaya nchini wameagizwa kusimamia kazi zinazofanywa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) ili kuleta matokeo tarajiwa katika kukuza ustawi wa uchumi nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo katika kikao cha Wakuu wa Wilaya kuhusiana na kujenga uelewa wa majukumu ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(Tarura) katika ukumbi wa Hazina Dodoma.
Agizo hilo limetolewa leo mjini Dodoma na waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Suleimani Jafo akifungua kikao cha wakuu wa wilaya nchini.
Jafo amesema “Nawaagiza wakuu wa wilaya nchini kote muende kusiamamia barabara hizo kwa ukaribu ili barabara zitakazo jengwa ziwe na ubora na zitakazo dumu kwa muda mrefu,”.
Amewaambia viongozi hao kuwa uanzishwaji wa Tarura utainua chachu ya
uzalishaji wa mazao kutokana na usafiri wa uhakika kwani mkulima atakuwa na uhakika wakusafirisha mazao, lakini pia itapunguza gharama za
usafiri na kuboresha hali za maisha za watanzania.
Ameeleza kwamba serikali imekuwa na changamoto kubwa ya wakandarasi wanaopatiwa kazi za ujenzi wa barabara kutokuwa waaminifu na kujenga chini ya kiwango, rushwa , hivyo ni kazi ya mkuu wa Wilaya kusimamia ili kubaini mapungufu hayo kwa haraka na kuokoa fedha za Serikali.
Amesema kuwa baada ya kuifahamu Tarura ni jukumu lao kuibua maovu kwa wafanyakazi wanaofanya maovu ili waweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma.
Amesema kuwa Wakuu wa Wilaya ni wawakilishi wa serikali katika maeneo yao, hivyo wanawajibu wa kusimamia kwa ukaribu zaidi katika usimamizi wa
mradi ya Ujenzi wa Barabara nchini.
No comments:
Post a Comment