Dkt. Oscar Kikoyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
Na Noel Rukanuga.
Baraza la Ushauri la Watumiaji
wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC) limewataka wamikiki wa
mabasi yaendayo mikoani kufuata masharti ya leseni zao na kutoza nauli zilizoidhinishwa
na mamlaka husika.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Katibu
Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Oscar Kikoyo, amesema kuwa wamiliki wote wa mabasi
wanapswa kufata sharia pamoja na kuwahimiza wafanyakazi wao wanaokata tiketi
katika vituo mbalimbali nchini kuwa waaminifu kwa waajiri wao na wateja wao.
Amesema kuwa sasa kuna wingi wa
abiria hao, ambapo kila mwaka mahitaji ya usafiri kwa kipindi hiki yanazidi
kuwa makubwa kuliko huduma ya usafiri uliopo na kusababisha baadhi ya watoa
huduma ambao sio waaminifu huchukulia kipindi hicho kama njia ya kuvuna zaidi.
“Baadhi ya watoa huduma wanakwenda
kinyume na masharti ya leseni zao kutokana na mahitaji makubwa ya usafiri na abiria
hukubali wenyewe kulipa zaidi kusudi wapate kusafiri jambo ambalo sio rafiki”
amesema Dkt. Kikoyo.
Amesema kuwa baraza linatoa
wito kwa watu wote wanaotarajia kusafiri kipindi cha mwisho wa mwaka kufanya
maandalizi ya safari zao mapema ikiwa ni pamoja na kufanya booking na/au kukata
tiketi zao mapema ili kuepukana na matatizo ya kulanguliwa tiketi.
Ameeleza kuwa ni vema abiria wote kutonunua tiketi za safari zao kutoka kwa wapiga
debe au vishoka katika eneo la kituo cha mabasi cha ubungo au vituo vingine
nchini kote.
“Baadhi ya watoa huduma
wanawakatalia abilia kutofanya booking mapema, kunasababisha abiria kurundikana
vituoni siku za safari bila sababu yoyote na hivyo kutoa mwanya kwa wapiga debe
na vishoka kuwalaghai abiria hao, tunaomba abiria watakaokataliwa kufanya
bookings zao mapema mwaka huu kutoa taarifa kwetu au kwa Mamlaka ya SUMATRA kwa
hatua zaidi” amesema Dkt. Kikoyo.
Hata hivyo baraza la SUMATRA limeendelea
kutoa wito kwa abiria wote kuhakikisha wanasafiri kwa tiketi yenye jina lao na
iliyoandikwa kiwango sahihi cha nauli uliyolipa.
Imeeleza kwa wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani kupitia umoja wao (TABOA) na watumishi wao kuzingatia kanuni usafirishaji (Transport
Licensing (Public Service Vehicles) 2017 (GN No. 421) hususani kanuni 25 (b)
(iii) na Kanuni 38 (1) (b).
Dkt. Kikoyo imeitaka TABOA
kuhakikisha madereva wao wanaendesha magari kwa mwendo unaokubalika. Kutokana kuna
taarifa kuwa kipindi cha Krismas mabasi mengi huenda mwendo kasi kusudi wageuze
siku hiyo hiyo kwa ajili ya kutengeneza fedha zaidi.
Amesema kuwa jambo hilo linaatarisha
usalama wa abiria, hivyo usalama wa abiria unapaswa kupewa kipaombele kuliko
fedha.
Wito wa Baraza kwa Mamlaka
zinazohusika:
1. Magari yanayopewa vibali
vya muda yafanyiwe ukaguzi wa kina kabla
ya kukata tiketi.
2.Watoa huduma wachache
hasa wale wanaopewa vibali vya muda waache mara moja kufanya udanganyifu katika
nauli.
3.Vibali vya muda mfupi ni
kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kuna usafiri wa kutosha kipindi hiki cha
Krismass na mwisho wa mwaka.
4. Abiria wote wawe makini
kwenye ukataji wa tiketi, hakikisha tiketi uliyopewa ina kumbukumbu zako sahihi
na nauli sahihi uliyolipa.
5. Kituo cha ubungo kina
vijana wanaobeba mizigo, kwanza kubalianeni bei kabla hajabeba mzigo wako, pili
hakikisha kijana anayebeba mizigo yako amekupatia kadi yake yenye namba
iliyoandikwa kwenye koti lake, nyuma na mbele na kwenye troli lake
No comments:
Post a Comment