Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya JUTA PLC Peter Isare
Baadhi ya bidhaa viroba vya uga na mchele kutoka kampuni JUTA zikiwa katika monyesho ya Pili ya Viwanda yanayofanyika jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba
WINGU LA HABARI
Na Noel Rukanuga
Wafanyabiashara pamoja na wakulima wametakiwa kuchangamkia fursa
kwa kujiunga na kampuni ya JATU PLC ambayo inawapa fursa watanzania katika
kujenga afya na kutokomeza umaskini kupitia kazi ya kilimo na masoko.
Kampuni hiyo ya JATU inawapa fursa watanzania katika masuala
ya kiuchumi kwa wanachama wake katika kununua shamba kwa ajili ya kilimo, kutoa
mkopo pamoja kuwa karibu na masoko.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika
maonyesho ya pili ya Viwanda, Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya JATU PLC Peter
Isare, amesema kuwa ndani ya kampuni hiyo wanafanya mambo makubwa matatu ambayo
ni rafiki kwa watanzania.
Amesema kuwa mambo hayo ni pamoja na shughuli ya Kilimo, viwanda
pamoja na masoko za bidhaa mbalimbali ambazo wanazalisha.
Isare amefafanua kuwa lengo leo ni kuzalisha bidhaa kuanzia
hatua ya kwanza hadi ya mwisho ambapo bidhaa inamfikia maraji.
“Kufanya hivyo inamsaidia mkulima kuondokana na mfumo wa
madalali baada ya mazoa yake kuwa tayari kwa biashara” amesema Isare.
Ameeleza kuwa mfumo wa madalali umekuwa mkubwa sana hivyo
wameamua kuwaandaa mkulima kuanzia mashambani na kuwasaidia kupata masoko kwa
bei rafiki.
Isare amesema kuwa kwa sasa wamefanikiwa kuwa na vituo vya
bidhaa katika mkoa wa Morogoro, Dodoma, Pwani, Dar es Salaam pamoja na
Zanzibar.
Hata hivyo amewataka watanzania wote kujiunga na kampuni ya
JATU ili kunufaika na faida mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa (wakala), kupata
mkopo, bima ya afya.
Kampuni JATU imekuwa na utaratibu rafiki kwa wakulima katika
kuhakikisha wanapiga hatua na kuwapatia mikopo ili kuendeleza shughuli za
kilimo hapa nchini.
Katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na viwanda wameweka
utaratibu wa kwa kila mtanzania kujiunga na JUTA PLC kwa kujaza fomu kwa
gharama ya Sh 10,000 na kupata fursa mbalimbali za kiuchumi.
JUTA kwa sasa inaendelea kulima na kuzalisha bidhaa
mbalimbali pamoja na kuuza kupitia wakulima,mawakala ambapo kila mmoja
ananufaika na faida ya kampuni.
No comments:
Post a Comment