Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akifafanua jambo
wakati akiongea na waaandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Tamisemi mjini
Dodoma.
Zaidi ya asilimia 98 ya wanafunzi wamechaguliwa kujiunga na masomo ya
kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza mwaka 2018 kati ya wanafunzi
650,862 waliofanya mthiani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka huu.
Akitangaza matokeo
hayo mjini Dodoma kwa upande wa Tanzania Bara waziri wa nchi ofisi ya rais
tawala za mikoa na serikali za mitaa Seleman Jafo, amesema kuwa idadi wa
wanafunzi mwaka huu imeongezeka.
“Wanafunzi 124,209 na
ni sawa na asilimia 23.58 ikilinganishwa na wanafunzi 526,653 waliochaguliwa
awamu ya kwanza kuingia kidato cha kwanza mwaka 2016,” amesema.
Amesema kuwa wanafunzi
1912 wenye uhitaji maalum (pupils with special needs) waliofaulu mitihani ya
darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka 2018
kwenye shule za sekondari za Serikali.
Jafo amefafanua kuwa
wanafunzi 11,173 sawa na asilimia 1.69 ya waliofaulu hawakupata nafasi ya
kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika awamu ya kwanza ya uchaguzi
kutokana na uhaba wa miundombinu ya elimu hususani vyumba vya madarasa kwenye
baadhi ya halmashauri ya Mikoa ya Lindi (170), Mbeya (3,092), Rukwa (4,091),
Manyara (1,268), Katavi (976) na Simiyu (1,576).
No comments:
Post a Comment