Mgombea wa chama tawala cha Kulmiye ameshinda uchaguzi wa urais katika eneo lililojitenga la Jamhuri ya Somaliland.
Mgombea huyu Muse Bihi Abdi alikuwa mwanajeshi wa zamani aliibuka mshindi kwa kujipatia asilimia 50 ya kura hizo.
Chama kikuu cha upinzani cha Wadani kimesema kuwa kulikuwa na udanganyifu wakati wa uchaguzi huo.
Hata hivyo watu kadhaa wameuawa kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi huku Bihi ni rais wa tano wa Somaliland tangu ilipojitenga na Somalia 1991, ambapo anakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo idadi kubwa ya watu wasio na ajira , kiangazi na kutotambuliwa kwa Somaliland. Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment