Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa mada katika Warsha hiyo iliyojadili mambo mbalimbali yanayohusu kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na salama kwa mama na mtoto nchini.
Jamii imehimizwa kumpeleka mzazi kwenda kwenye vituo vya Afya ambavyo vina wataalamu ,kwani hatua hiyo ndio njia ya kusaidia kuondokana vifo hivyo,huku Sseri8kali ikitakiwa kongeza bajeti katika Wizara ya Afya upande wa afya ya Mama na mtoto.
Hayo yamesemwa leo na Mratibu Taifa wa Muungano wa UtepeMweupe na Uzazi Salama, Rose Mlay, wakati wa mkutano wa wadau wakati wa Mkutano wa Wadau wa Afya na Mama na Mtoto uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kupoteza mtoto na mama ni ajali ambayo inatokana na kukosekana kwa huduma sahihi wakati wa kujifungua.
Amesema mkutano wadau ni pamoja na kujadili takwimu za Afya ya Mama na Mtoto pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya uzazi.
Ameongeza kuwa kwa sasa vifo vya wakina Mama vimeongezeka kutoka kwa vifo 24 vya wakinamama kwa siku hadi kufikia vifo 30 kwa siku huku akisema ongezeko hilo limechangiwa na wakina Mama kujifungulia sehemu zisizo salama,
“Ripoti inaonyesha vifo vinaongezeka kutokana na kukosekana kwa vituo vya afya vyenye pamoja na wataamu kama nyumbani na kwenye vituo visivyo na watalaamu,unakuta sehemu hakuna vifaa vya kumsaidia Mama ili aweze kujifungua salama,na hii inasababisha vifo hivi kuongekezeka”
“.Amesema jamii kama ingekuwa inampeleka Mzazi kwenye vituo vya afya vyenye ubora basi vifo hivi vingepungua ikiwezekana kumalizika kabisa”Amesema Mlay.
Mlay amesema Takwimu za hapo awali zilionyesha kuwa takribaniwanawake 8000 hufaliki kila mwaka kwa sababu ya Matatizo yanayotokana na Mimba na Uzazi lakini Takwimu hizo zimeongekeza hadi kufikia zaidia ya elfu 10 kwa mwaka .
Nao baadhi ya Wadau mbalimbali waliokuwepo kwenye semina hiyo ,wameitaka serikali kuhakikisha inaongeza bajeti kwenye sekta ya Afya ambayo itavisaidia kwenye vituo vya Afya kuwepo kwa wakunga wenye welevu na ujuzi ambao watasaidia kupunguza vifo hivo
No comments:
Post a Comment