Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Patrobas Katambi amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aliyekuwa Mwenyekiti Bavicha Patrobas Katambi (Kushoto)
Katambi ametangaza kujiondoa Chadema leo jijini Dar e Salaam katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM unaoendelea Ikulu chini ya Mwenyekiti wake Rais John Magufuli.
Katambi alikuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akikabiliana na Stephen Masele (CCM) ambaye aliibuka mshindi huku Katambi akidai kuibiwa kura katika uchaguzi huo.
Mbali na Katambi makada wengine wa CHADEMA wameamua kurudi CCM.
No comments:
Post a Comment