Bw Valllenstein S/O Alvarez Santillan akiwa katika. |
Na Noel Rukanuga
Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Kuzui na Kupambana na
Dawa za Kulevya linamshikilia Valllenstein S/O Alvarez Santillan raia wa Peru
(35) kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za kulevya aina ya cocaine zenye uzito wa
kg 1.42 ambapo ni kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkuu wa kitengo
cha kuzuia dawa za kulevya ACP Alhaji Kabaleke, amesema kuwa novemba 16 mwaka
huu walimkamata Santillan katika uwanja cha ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere
akiwa na dawa za kulevya paketi 31.
ACP Kabaleke amesema kuwa kukamatwa kwa mtu huyo kumetokana
na kupata taarifa kuwa kuna raia wa peru ambaye anatoka nchini Brazil
inasadikika anajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
“Baada ya kupokea taarifa niliunda kikosi kazi ambacho
kiliweza kufika mara moja uwanja wa mwalimu Julius Nyerere na kufanikiwa
kumkamata akiwa na dawa za kulevya” amesema ACP Kabaleke.
ACP Kabaleke amefafanua kuwa mtuhumiwa huyu alitokea nchini
Brazil ambapo alidhificha dawa za kulevya kitaalamu na kusababisha mashine za
kukagua uwanja wa ndege kushindwa kubaini uwepo wa dawa za kulevya.
Ameeleza kuwa mtuhumiwa muda wowote atakifishwa mahakamani
kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kikosi cha kuzuia na kupambana na dawa za kulevya
kinaendelea na vita kwa watuhumiwa, wanaojihusisha na uingizaji, usambazaji na
watumiaji ambo wanatumia viwanja vya ndege, mipaka mbalimbali ya nchi.
Kwa mujibu wa takwimu za ukamataji wa kesi za dawa za kulevya
katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi novemba mwaka huu, imebainika kuwa
dawa za kulevya aina ya heroin zilizokamatwa ni kg 1.17.
Huku cocaine zikiwa kg 1.487, bhangi kg 26, 501.87, Mirungi
kg 814. 76 pamoja na mashamba ya bhangi yaliochimwa moto yakiwa hekari 182.25
katika mikoa yote.
Hata hivyo wananchi wametakiwa kuendelea kutoa taarifa ili
kutokomeza mtandao wa dawa za kulevya hapa nchini.
No comments:
Post a Comment