Mamlaka ya Maabara ya Mkemia wa Serikali imeanza kuimarisha Maabara zote za kanda kwa lengo la kuwasogezea karibu huduma wananchi ambao awali walikuwa wanalazimika kufata kwenye Ofisi za Mkemia Mkuu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Meneja Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Cletus Mnzava, amesema kuwa hapa nchini kuna Maabara sita za kanda.
Manzava amesema kuwa kanda hizo ni pamoja na kanda ya ziwa inayohudumia mikoa ya Mwanza, Bukoba, Simiyu, Mara, Shinyanga, Geita na Kigoma.
Kanda ya Kaskazini inayohudumia Mkoa wa Arusha, Kilimanjaro, Tanga pamoja na Manyara, Kanda ya kati inayotoa huduma Mkoa wa Dodoma, Singida, Morogoro, Tabora na Iringa.
Kanda ya Mashariki inayohudumia Mkoa wa Dar es Salaam pamoja Pwani wakati kanda ya Nyanda za juu kusini inajumuisha mikoa wa Mbeya, Katavi, Songwe na Rukwa.
Kwa upande wa kanda ya Kusini itaendelea kuhudumia mkoa wa Lindi, Mtwara pamoja na Songea.
Amesema kuwa kwa sasa mamlaka imejipanga kuimarisha utendaji kazi wa kanda zake kwa kuzipatia vifaa vya maabara vya kisasa kwa kanda ambazo tayari zina maabara.
“Tutajenga majengo ya kudumu ya Ofisi za Mamlaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika kanda ili kuweza kuwekeza vifaa vya kudumu katika ofisi hizo badala ya sasa hivi inakuwa ngumu kwani muda mwingine unaweza kuweka mitambo ambayo mtatakiwa kuhamisha” amesma Mnzava.
Amesema kuwa lengo kuu la kuimarisha Maabara za kanda ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuweza kuhudumiwa bila kulazimika kuja kufata baadhi ya huduma kwenye Ofisi za Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment