
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe.Isaya Mwita akizungumza na Madiwani waliohudhuria kwenye baraza hilo
MWAMBA WA HABARI
Jiji la Dar es Salaam limedhamiria kufanya mradi wa uhamishaji wa kituo cha mabasi cha ubungo kwa lengo la kupisha utengenezwaji wa daraja la Ubungo interchange
Hayo yameelezwa leo na Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita katika Baraza la Madiwani ambacho kikao hicho kilikuwa na lengo la kila kamati kutoa taarifa za mipango kazi katika ufanikishaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Mwita amesema mpaka sasa wamefanya mazungumzo na wadau mbalimbali ikiwemo Sumatra,Tanrod,Taboa pamoja na jiji ili kuhakikisha wanafanikisha kuhamisha kituo hicho.
Amewataka wananchi kuhakikisha wanaonyesha ushirikiano kwa viongozi wao kwa kuupokea mradi huo kwani unalenga kuwa na maslahi bora kwa nchi.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Temeke Abdala Chaurembo amesema kuwa zaidi ya miaka mitano iliyopita mipango ya serikali ilionyesha kwamba eneo hilo patajengwa interchanje.
Hata hivyo jiji la Dar es Salaam limejipanga kuhakikisha linatekeleza mikakati ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo hivyo wananchi wametakiwa kuwa bega kwa bega na viongozi wao ili waweze kufanikisha kwa wakati malengo waliyojiwekea ya kuboresha jiji hilo.
No comments:
Post a Comment