Na
mwandishi Wetu
Idadi
ya mauzo katika soko la hisa imeongezeka kwa asilimia 76% kutoka Sh billion 2.8
hadi kufikia bilioni 4.9.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa mauso wa soko la hisa (DSE) Patrick Mususa,
alisema kuwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki hii imeshuka kwa
asilimia 20% hadi kufikia Sh Milioni 2.2 kutoka Sh Milioni 2.8
kwa wiki iliyopita.
Hata
hivyo alibainisha kuwa Kampuni tatu yanayohongoza
kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni pamoja na benki NMB kwa asilimia
48% , CRDB kwa asilimia 38% pamoja na kampuni ya SWISSPORT kwa asilimia 10%.
Aidha ukubwa wa mtaji wa soko umeongezeka asilimia
0.5% hadi kufikia sh Trilioni 22.1 kutoka sh Trilioni 22, Katika mtaji wa
makampuni ya ndani umepungua kwa asilimia 0.1% hadi kutoka shTrilioni 8.4
hadikufikia Trilioni 8.5.
Katika Viashiria Sekta ya huduma za kibenki na kifedha wiki hii
imeshuka kwa pointi 10.36 baada ya bei kushuka kwenye kaunta za CRDB benki
1.33% na Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imeshuka kwa pointi 16.75
baada ya bei kushuka kwenye kaunta ya SWISSPORT (0.59%).
Akizungumzia Shindano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (DSE Scholar Investment
Challenge 2016) Bw Msusa alisema kuwa Maendeleo
ya Shindano hilo yanakwenda vizuri na
hadi sasa kuna idadi wanafunzi 3,160 kutoka vyuo mbali mbali ambao wanaendelea
na ununuzi na uuzaji wa hisa na bondi katika DSE Scholar Investment Challenge
2016.
Katika
shindano hilo kuna Vyuo vitano (5) ambazo vinavyoongoza kwa idadi ya wanafunzi
waliofikia mia tano bora (Top 500) kwenye shindano hilo. Vyuo hivyo ni pamoja IRDP DODOMA - inaongoza na
wanafunzi 75, SAUT - inafwata na wanafunzi 66,UDSM - inafwata na wanafunzi 50
pamoja na IFM ikiwa na wanafunzi 43.
Katika
hatua nyingine DSE inaendelea kuuza hisa zake ambapo mtu yoyote anaweza kununua na kuuza kwani hisa moja inauzwa
kuanzia sh 500 na mtu anaruhusiwa
kununua hisa hadi 100.
No comments:
Post a Comment