Dar Brew yazindua muonekano mpya wa Chibuku Super. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, May 31, 2016

Dar Brew yazindua muonekano mpya wa Chibuku Super.

Na Mwandishi Wetu
Meneja masoko wa DarBrew Oscar Shelukindo katikati akizungumza jambo  kwenye uzinduzi wa chupa mpya yenye ujazo wa 750Mls ,Kulia ni Meneja mauzo na usambazaji wa DarBrew Fred Kazindogo  na kushoto ni mwakilishi wa mauzo Agripina Kusa  pamoja na  Neema Mvungi mwenye fulana  wote wakiwa katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Dar Brew imezindua chupa mpya ya bia ya asili ya Chibuku Super yenye ujazo wa milimita 750, ambayo mtumiaji halazimiki kurudisha chupa pale anapoitumia.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Dar Brew, Oscar Shelukindo alisema, bia hiyo iliyopo katika chupa nzuri ya plastiki inayovutia, itauzwa kwa bei ya Sh 1,000 tu kwa kila chupa.

“Leo  ni siku ya furaha kubwa sana kwetu Dar Brew na kwa watumiaji wote wa bia, kwani tumefanikiwa kuzindua chupa hii itakayouzwa kwa bei nzuri ya Sh 1,000 tu na kwa ujazo unaotosheleza” alisema.

Shelukindo alibainisha kuwa Bia hiyo imetengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, na kuhakikishia watumiaji wanatumia bei ikiwa na ubora wa hali ya juu.


Shelukindo alisema, bia hiyo imetengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mtama ulio bora, hivyo kuna kila  sababu kwa Watanzania kujivunia kilicho chao na kukumbuka asili yao, kwani hii ni bia yao ya asili.

“Chibuku Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachokufanya uitumie kwa muda mrefu ukiwa na marafiki, lakini inakupa lishe nzuri kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika nafaka zilizotumika kutengeneza bia hii.”

Naye Meneja Mauzo na Usambazaji wa Dar Brew, Fred Kazindogo alisema, bia hiyo itaanza kupatikana nchi nzima katika baa, maduka makubwa (Super Markets), katika maduka ya jumla na rejareja na sehemu zinazouzwa vileo kuanzia leo.

“Tunatarajia wateja na wapenzi wa bia wataifurahia chupa hii mpya na kwa wauzaji wa jumla, tunaamini watahamasika kuuza Chibuku Super kwani ina faida nzuri na haina usumbufu wa kununua chupa,” alisema.

Kazindogo alisema, ana imani kubwa wapenzi wa bia wataipokea kwa shangwe na wataitumia ili kuonesha wanajali asili yao. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here