Taifa starz kuminyana na Mapharao wa Misri Juni 4 mwaka huu. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, May 31, 2016

Taifa starz kuminyana na Mapharao wa Misri Juni 4 mwaka huu.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'taifa stars'' ambacho kinatarajia kushuka dimbani  hivi karibuni kuminyani na Mapharao wa Misri  jijini Dar es Salaam.






TIMU ya Taifa ya mpira wa mikuu Tanzania ''taifa stars'' wanatarajia kushuka dimani juni 4, mwaka huu kuminyana na Mapharao wa Mirsri katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kushirika michuano ya kombe la mataifa Afrika (AFCON) ambao utapigwa majira ya saa 10 jioni katika uwanja wa taifa uliopo jijini Dar es Salaaam.

Katika  mchezo huo utakaochezeshwa na marefa wanne kutoka Gabon ambapo  mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.

Laikini  Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia leo ambapo wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.

Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jMei 30, 2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Wakati huo huo: Timu ya soka Taifa ya Wanawake ya Tanzania – Twiga Stars, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rwanda, utakaofanyika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda.


Rwanda wameomba mchezo ufanyike ili kukiimarisha kikosi chao pamoja na kuboresha uhusiano wa nchi ambazo zote ni nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here