Kamanda wa
ngazi ya juu wa kundi la al-Shabaab
anayeshitakiwa kupanga mashambulizi ya mwaka 2015
dhidi ya chuo kikuu cha Garissa nchini
Kenya ameuwawa katika shambulio la majeshi maalum
kusini mwa Somalia.
Serikali ya
Kenya imesema Mohammed Kuno alihusika katika
kupanga shambulio la Aprili 2015 ambalo
lilisababisha vifo vya watu 148.
Operesheni hiyo ,
iliyofanywa na wanamgambo wanne wa al-Shabaab ,
ilikuwa shambulio baya kabisa la kigaidi
nchini Kenya tangu pale al-Qaeda waliposhambulia ubalozi
wa Marekani mjini Nairobi mwaka 1998, na kuuwa watu 213.
Chanzo DW.
No comments:
Post a Comment