Na Mwandishi wetu
KESI inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kilimanjaro ,Thomas Ngawaiya juu ya kujenga ujenzi wa ghorofa
bila kufata sheria, Kesi hiyo imeendelea leo katika mahakama ya hakimu mkazi
kisutu iliyopo jijini Dar es Salaaam.
Wakili upande wa utetezi, Jonathan Mulinga ameitaka
mahakama isizogeze mbele kesi hiyo ile wamalizane na upande wa mashtaka kwa
kujadiliana na kupata muafaka nje ya mahakama hiyo.
Hata hivyo Hakimu Mkazi Respicios Mwijage amehailisha kesi hiyo mpaka
itakapotajwa tena Juni 16 Mwaka huu.
Ngwaiya
alifikishwa katika mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kufanya
shughuli za ujenzi wa ghorofa kinyume cha sheria namba 17 kifungu 22(4) ya
ukandarasi ya mwaka 1997.
KATIKA
hatua nyingine Mtu
mmoja aliyefahamika kwa majina Mbaraka Mtambo (50) amefikisha katika mahakama ya
hakimu mkazi kwa kosa la kusafirisha nyara za serikali alizokamatwa nazo katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julias nyerere.
Akisoma
mashitaka hayo na Wakili wa serikali Hanorin Mushi Wakili mbele ya Hakimu Mkazi Helen Liwa amesema kuwa
mtuhumiwa huyo Tarehe 7 Mei mwaka huu alikamatwa katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere na magamba mawili ya Kasa ambayo ni
Mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mshitakiwa amekiri kutenda kosa hilo, hivyo Hakimu Liwa alimwambia kuwa hatipata dhamana kutoka na kesi hiyo, ambayo itatolewa uamuzi kesho tarehe 19 Mei.
No comments:
Post a Comment