Na Mwandishi wetu
Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC), kimesikitishwa na
vitendo vinavyofanywa na baadhi ya watu juu ya kusambaza picha za kutisha
ikiwemo picha za marehemu katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ya
kijamii bila kijali kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Haya yamebainisha leo
na Mkurungenzi Mtendaji (LHRC), Dkt Helen kijo Bisimba, ambapo amesema kuwa
kumekuwa na matukio kadha yanayofanywa na watu juu ya kurekodi picha ambazo sio
nzuri kwa mujibu wa sheria.
Dkt kijo amesema kuwa Mei 4 mwaka huu, katika Mkoa wa Pwani
Wilaya ya Bagamoyo pisha za Miili ya
marehemu mama na mtoto ambayo majina yao yamehifaziwa, zilisambazwa katika mitandao ya kijamii
zikionyesha majeraha ya kutisha
kutokana na kitendo cha kinyama
walichofanyiwa.
Katika tukio la pili amebainisha kuwa ilitokea Mkoa wa
Kilimanjaro mwaka huu, ambapo picha za maiti ya mtoto aliyeuwawa na mama wa kambo zikionesha akiwa
ndani ya jeneza.
Hata hivyo maeneo ya kibamba jiji Dar es Salaam, January mwaka
huu Picha za utupu za mwanamke aliyesemekana kuwa ni msukule aliyekutwa kwenya
kisima,na picha hiyo ilizambaza katika mitandao ya kijamii.
Amesema kuwa hayo ni baadhi ya matukio, hivyo jamii inapaswa
kutambua vitendo hivyo ni udhalilishaji
na kinyume cha sheria, kwani kwa mujibu wa haki ya kikatiba ibara ya 16 ya
katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 kila mtu ana haki ya kikatiba ya kuthamini
utu wake kwa kuwa faragha akiwa hai au amefariki.
No comments:
Post a Comment