Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista
Mhagama,akizindua ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya
kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam.
Utafiti
uliofanyika hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umebaini kwamba
asilimia 71 ya watanzania wanatumia muda mwingi kufanya shughuli zisizokuwa za
uzalishaji mali wala tija binafsi kwao na Taifa kwa ujumla
Akizundua
taarifa ya utafiti huo jijini Dar es
salaam Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Ajira,Vijana na watu
wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa idadi hiyo hufanya kazi
zisizoleta tija kwao na taifa na muda mwingi huutumia kujihudumia binafsi kwa
kulala na starehe nyingine.
Ameeleza
kuwa takwimu hizo zinaonesha wazi ni kwa namna gani watanzania wanashindwa
kujishughulisha katika kufanya kazi zenye kuwaingizia kipato na badala yake
wanatumia muda wao mwingi kufanya shughuli zisizo za uzalishaji hasa kufanya
starehe mbalimbali.
“
Ndugu zangu watanzania unakuta mtu amekaa baa au anacheza “poll table” kuanzia
asubuhi mpaka jioni na hujui anafanya kazi gani ya uzalishaji, ndugu zangu
tuone aibu basi tujishugulishe tulijenge taifa letu ili kujiletea maendeleo
yetu na nchi yetu.”
Aidha,
matokeo hayo yamebainisha kuwa asilimia 18.5 ya wananchi wanafanya kazi za uzalishaji
na asilimia 10.6 ni wale wanaofanya shughuli za nyumbani zisizo na malipo huku
uchambuzi wa kijinsia ukionesha kuwa wanaume asilimia 23.8, wanatumia muda
mwingi kwenye shughuli za kiuchumi ikilinganishwa na asilimia 13.5 ya wanawake.
Amefafanua
kuwa wanawake ambao ni asilimia 16.5 katika utafiti huo wanatumia muda mwingi
kufanya kazi za nyumbani zisizo na malipo ikilinganishwa na asilimia 4.4 ya
wanaume.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisa ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa
amesema kuwa upatikanaji wa Takwimu hizo utaisaidia Serikali kupata mbinu
sahihi za kuondokana na tatizo la ajira nchini kwa kuunganisha nguvu kutoka
sekta isiyo rasmi ili kuleta changamoto katika soko la ajira nchini.
Amesema
kuwa hii ni mara ya tano Tanzania inafanya utafiti huo na kubainisha kuwa
ulianza mwezi Januari hadi Desemba, 2015 ukitumia sampuli ya
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyotumika kupata taarifa sahihi
ya takwimu hizo.
Aidha,
amebainisha kuwa ili kufanikisha utafiti huo NBS imeshirikiana na wadau
mbalimbali ikwemo Wizara ya kazi na Ajira,Shirika la Kazi Duniani (ILO),Benki
ya Dunia (WB),Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) na Asasi zisizo za Kiseikali.
Chanzo; Mwamba wa habari.

No comments:
Post a Comment