Kuna maneno kuwa kiungo wa timu ya ufaransa Paul Pogba
kuelekea Barcelona au Manchester City lakini kiungo huyo atabaki kwa vibibi
vizee vya turini katika kipindi hiki”,Alisema Mino Raiola.
Mino Raiola ambaye ni wakala wa kiungo huyo wa Juventus
amesema Paul Pogba mwenye miaka 22 ataondoka katika ligi hiyo ya Serie A
mwishoni mwa kipindi cha mwaka 2015.
Mino Raiola ambaye pia ni wakala wa wachezaji Zlatan
Ibrahimovic na Mario Balotelli, amesema mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya
Ufaransa anafurahia maisha aliyonayo katika klabu yake ya Juventus.
Amesema hawezi kuondoka katika kipindi cha usajili wa
january ila hadi mwakani mwezi wa 7 na muda ukifika wa kuondoka ataondoka kama
akhitaji kuondoka klabuni hao.

No comments:
Post a Comment