Watanzania wametakiwa kuchagua wagombea katika nafasi ya Udiwani, Ubunge pamoja na Urais wenye vigezo vya kuongoza na kujali maslahai ya taifa na sio chama chake.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Kampeni na uchaguzi wa
NCCR-MAGEUZI Faustin Sungura ambapo alisema kuwa wamefatilia kwa umakini wa hali ya juu kampeni za
uchaguzi wa wagombea wa vyama mbalimbali hapa nchini na kubaini baadhi ya wagombea
hawakubaliani na sera za chama chake kutokana ufisaidi unaofanyika.
Sungura alisema kuwa kutoka na sera anazotumia mgombea wa
Urais kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Dkt John Pombe Magufuli inonyesha kuwa hata yeye hapendi
mwenendo wa chama chake.
Alisema mikutano yake ya kampeni ulezea maovu ya yanayofanya
na Serikali CCM kwani baadhi ya mikutano hiyo alisema kuwa
nikiwa Rais itakuwa mwisho serikali kuwakopa wakulima,kwa sababu ni
aibu, nikiwa Raisi itakuwa marufuku wagonjwa kwenda hospitalini kuandikiwa dawa
na kuelekwezwa wakazinunue kwenye
maduka ya dawa.
Sungura alisema kuwa katika hali
ya kawaida , maneno hayo au
hutuba kama hizo zilitakiwa
kuchukuliwa hatua na chama chake
kutokana na ukimya wa chama, Dkt
Makufuli huenda angetekeleza yaliyo
moyoni mwake juu ya chama chake.
‘’ Kutokana na sera za Dkt Magufuli za kuikosoa serikali ya CCM
, hakuna sababu za msingi za kuendelea kuwachagua wagombea wa Chama cha
Mapinduzi , badala yake tunawaomba
wapiga kura wachague wagombea kutoka kambi ya upinzani’’ alisema.
Mbali na hayo Sugura amebainiisha kuwa kwa mujibu wa sheria
mpiga kura anahaki ya kumchagua mgombea yoyote anayemtaka
pamoja na kubaki au kuondoka kwenye eneo la mduara wa mita 200 kutoka kwenye kituo cha
kupiga kura.
Hata hivyo amefafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya
uchaguzi 104(1), kinakataza kufanya kampeni, kuvaa sare ya chama, au kufanya ishara inayoashiria kumfanyia kampeni mgombea wa siasa, na kifungu cha 126 cha sheria ya uchaguzi kinasema
maelezo yoyote yanayokizana na sheria yanayotolewa
na tume ya uchaguzi ni batili, na
Maelekezo ambayo yasiyo halali kwani
yanalenga kuwaogopesha wapiga kura na kutoa mwanya kw Chama cha CCM kuchukua
madaraka kwa kwa uwepesi.
Sanjali na hayo alisema
kuwa Mamlaka ya kituo cha kupiga kura yanaishia kwenye mipaka ya kituo cha kupiga kura tu,na kifungu cha sheria cha
104(1) cha uchaguzi kinatoa eneo
la mita 200 tu kutoka kituo cha kupiga kura, hivyo mtu yoyote akiamua kukaa
nje ya mita 200 bila kufanya fujo akiwa amekaa
inakubalika kwa mujibu wa sheria na hawezi
kuhesabiwa kuwa amevunja sheria.
‘’ NCCR-Mageuzi hatupo tayali kuona baadhi ya watu wanatumia
vibaya madaraka ya umma kukisaidia chama kuendelea kuwanyonya watanzania’’
alisema.
Sugura amewaomba watazania kwenda kupiga kura Oktoba 25 mwaka
huu na kuchagua wagombea wa wote wa Umoja wa Katiba UKAWA katika ngazi ya Udiwani,
Ubunge pamoja na Urais.
No comments:
Post a Comment