VITA VYA A WENYEWE KWA WENYEWE NCHINI SYRIA, KUTAFUTIWA JIBU. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, October 23, 2015

VITA VYA A WENYEWE KWA WENYEWE NCHINI SYRIA, KUTAFUTIWA JIBU.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Segej Lawrov wanakutana mjini Vienna Austria kwa ajili  ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Nchi hizi mbili zina misimamo tofauti kuhusiana na mzozo wa Syria ambapo Marekani inamtuhumu rais Bashar al Assad kuhusika na matumizi ya nguvu dhidi ya wakazi wa nchi hiyo pamoja na kuziendeya kinyume haki za binaadam.

Lakini Urusi ni mshirika mkubwa wa Assad na wanataka kwa kila hali aendelee kuwepo madarakani uku Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power amekumbusha muda mfupi kabla ya mazungumzo ya Vienna kuanza,kwamba wasyria 85 elfu wamefukuzwa pekee katika kipindi cha siku chache zilizopita.


Baada ya mazungumzo yao,mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani na Urusi watakutana kwa mazungumzo ya pande nne pamoja na wenzao kutoka Uturuki na Saud Arabia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here