WAANDISHI WA HABARI WAPASWA KUJITOKEZA TUZO ZA UMAHIRI (EJAT) - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, October 17, 2015

WAANDISHI WA HABARI WAPASWA KUJITOKEZA TUZO ZA UMAHIRI (EJAT)

Washindi wa tuzo zilizopita za umahiri wa Uandishi wa habari
(EJAT)











Na Noel Rukanuga.
Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Umahiri za uandishi wa habariTanzania (EJAT) imezindua rasmi tuzo hizo na kuwataka waandishi wa habari kujitokeza kwa wingi kwa kuzishindanisha kazi zao katika makundi mbalimbali.

Akizungumzia tuzo hizo wakati wa uzinduzi Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya (EJAT) Kajubi Makajanga  ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) alisema kuwa katika tuzo za mwaka huu wameongeza makundi mawili mapya ambayo ni habari za kodi pamoja na habari za manunuzi ya umma , lengo ikiwana ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi na kukusanya.

‘’Tumeanzisha makundi hayo mamili ili kutoa elimu kwa jamii ikiwemo kuwatia hamasa waandishi wa habari kuwa kuandika Zaidi huhusu sekta ya  Manunuzi ya umma ambayo inachipukia hapa nchini na kujenga  tabia ya uwajibikaji’’alisema.

Aidha alisema kuwa  baada ya kuongezeka makundi mawili mapya yatakayoshindanishwa na kufanya kuwe na idadi ya makundi 22 ambayo ni Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi na Biashara, Habari za Michezo na utamaduni, Habari za Mazingira, Habari za Afya, Habari za Watoto, Habari za VVU/UKIMWI, Habari za Utawala Bora, Habari za Jinsia, Habari za Sayansi na Teknolojia, Habari za Afya ya Mama na Mtoto, Habari za Uchunguzi, Habari za Elimu, Habari za Watu Wenye Ulemavu, Habari za Utalii na Uhifadhi, Mpiga picha Bora-Magazeti, Mpiga Picha Bora- Runinga, MChora Katuni Bora, Habari za Kilimo, Afya ya Uzazi kwa vijana, Habari za Gezi, Mafuta na Uchimbaji wa Madini, Habari za Kodi na Ukusanyaji wa Mapato, Habari za Manunuzi.

Washindi kutoka makundi mbalimbali watazawadia vyeti, tuzo na zawadi nyingine ambazo zimeandaliwa, na Tamasha la EJAT ambalo limepangwa kufanyika April 29,2016.

Hivyo Waandishi wa habari wanakaribishwa kuanza kuwakilisha kazi zao kuanzia Oktoba 16,2015 hadi Februari 15,2016 na kazi hizo ziwe zimefanyika mwaka huu 2015.

Katika hatua nyingine Bw Mukajanga amewataka waandishi wa habari kuwa makini katika uandishi wao hasa kipindi hiki cha uchaguzi ambao umeonekana kuwa na changamoto nyingi.

‘’ kiukweli uchanguzi unachangamoto nyingi, ili kuhakikisha tunazikali hizo changamoto tunapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma lengo ni kuwasaidia wapiga kura kuwa na uelewa mkubwa juu ya wagombea wa nafasi mbalimbali’’ alisema Mukajanga.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here