 |
| Mchezaji wa mpira wa vikapu Lamar Odom. |
Mchezaji
wa zamani wa mpira wa vikapu katika ligi ya NBA nchini Marekani Lamar Odom
hatimaye amepata fahamu siku tatu baada kuzirai ndani ya danguro katika jimbo
la Nevada.
Chanzo cha habari kimesema kuwa
bwana Odom alizungumza na kutoa maamkuzi ya kidole katika kitanda chake cha
hospitalini.
Alikuwa katika mashine ya
usaidizi baada ya kupatikana siku ya jumanne akitokwa na damu puani na mdomoni.
Wafanyikazi
wa danguro la Love Ranch,huko Crystal,Nevada wamesema kuwa bwana Odom alikuwa
katika danguro hilo kwa siku kadhaa na amekuwa akila dawa za kulevya aina ya
cocaine .
No comments:
Post a Comment