WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA WAFUNDWA, WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI YAO. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, October 23, 2015

WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA WAFUNDWA, WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI YAO.

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari za uchaguzi bila upendeleo wowote,wakati huu wakampeni na wakati wa zoezi la uchaguzi utakaofanyika octoba 25 mwaka huu,ili kuliepusha taifa kuingia katika machafuko ya kisiasa.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa habari maelezo Assa Mwambene alipo kutana na waandishi wahabari kuzungumzia mstakabali wa taifa katika kipindi  hiki, ambapo ameleeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu umekuwa na mwamko ana ari kubwa kutoka kwa wananchi  hivyo amewaassa kuzingatia maadili na miiko ya kazi yao ili kila pande zipate haki sawa.

Aidha Mmwambene amesema nchi nyingi jirani na Tanzania kama,Rwada ,Burundi na kenya ziliingia katika machafuko  huku riport zikieleza kuwa machachafuko hayo kwa sehemu kubwa yalichangiwa na vyombo vyahabari  hivyo nivema kuitunza heshima ya Tanzania kimataifa kwakuwa ina sifika kuwa ni kisima cha Amani na kimbilio la nchi jiran.


Pamojana hayo amewataka waandishi wa habari wa kimataifa kufuata taratibu za tume yaTaifa ya uchaguzi zilizo wekwa ili kuondoa usumbufu utakao weza kujitokeza, na pia amewatakawata watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kupata viongozi wanaowataka na wadumishe Amani kwa muda wote wa zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here