| Meneja wa Soko la hisa (DC) Patric Mususa. |
Idadi ya mauzo katika
soko la hissa (DC) imepanda mara tatu kutoka 8.5 kwa wiki iliyopita hadi kufikia bilioni 24. 3
kwa wiki hii.
Akizungumza na Wingu la habari
meneja wa soko hilo Patric Mususa amesema kuwa pia idadi ya hissa zilizonunuliwa na kuuzwa katika
soko imeshuka kutoka milioni 14 kwa hadi kufika hadi kufukia milioni 10 wiki hii.
Aidha amebainisha kuwa Kampuni tatu zinazoongoza katika soko hisa zake kununuliwa na kuuzwa ni pamoja na Baki
ya CRDB inayoongoza kwa 86%, TBL ikiwa na 10% uku Twiga Cement ikishika nafasi ya tatu ikiwa na 1.4%.
Mususa amsema mtaji wa soko umeendelea
kubaki palepale trilioni 21.1, na mtaji wa makapuni ya ndani ukiwa trilioni 9.7 na kuongeza kuwa baadhi ya Makampuni ikiwemo DCB baki kwa 1.7% pamoja na TBL kwa 1.3%.
Na kiashiria katika sekta
ya viwanda kimepanda kwa point 27 kikiwa kimechangiwa na punguzo bei kwenye
kaunta ya TBL pamoja na kampuni ya twiga cement ,Wakati kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na kifedha
kimepanda kwa point 13, kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya katika kaunta
ya DCB baki pamoja baki NMB .
Uku kiashiria cha sekta
ya huduma za kibiashara kikishuka kwa point 20 kikiwa kimechangiwa na punguzo
la bei ya katika kampuni SWISSPORT kwa 0.68%.
Mususa amebainisha kuwa huduma ya kununua na kuuza hisa kwa
njia ya simu ya mkononi inaendelea vizuri mpaka muda huu kuna idadi ya watu Zaidi 1000
wanaendelea kufaidia na huduma hiyo , nakuwataka wanchin pamoja na taasisi mbalimbali kutumia huduma hiyo kwa kupiga namba*150*36#.
No comments:
Post a Comment