![]() |
| Gari aliyokuwa amepanda Mchungaji Mtikila. |
Mwanasiasa
mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic Party (DP),
Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa
katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze
mkoani Pwani alfajiri ya leo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amesema kuwa Mchungaji Mtikila Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 alfajiri ya leo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze.
Amesema gari alilokuwa amepanda Mtikila lilikuwa linatoka mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam, ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wanne ambapo wengine watatu wamejeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani kwa ajiri ya matibabu.
Kwa habari zaidi endelea kufuatilia habari zetu .

No comments:
Post a Comment