MCHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU NATHANIEL KERR AFUNGWA JELA MWAKA MMOJA - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, October 1, 2015

MCHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU NATHANIEL KERR AFUNGWA JELA MWAKA MMOJA

Mchezaji wa soka Nathaniel Kerr





Mchezaji soka mmoja nchini Uingereza amefungwa jela mwaka mmoja kwa kosa la kumvunja mguu mchezaji wa klabu pinzani kwa kumkanyaga mara kadha wakati wa mechi.
Nathaniel Kerr mwenye umri wa miaka 24, alikiri mashtaka mbele ya hakimu katika mahakama mjini Manchester, Uingereza.
Mchezaji aliyeumizwa Stuart Parsons, 30, alikuwa akijibizana na mmoja wa mchezaji mwenzake Kerr kwenye mechi ya ligi ya Sunday muda mfupi kabla ya kisa hicho uwanjani katika eneo la Stockport.
Kerr alimkanyaga Parsons mara kadha hadi mguu wake ukavunjika na ilimbidi kufanyiwa upasuaji na kukaa wiki kadha hospitalini.
Parsons alipokuwa amelala uwanjani akiwa na maumivu tele, Kerr alimwambia mwenzake kwa sauti: “Nimefanya haya kwa ajili yako”
Konstebo wa polisi Louise Spencer, wa kikosi cha polisi cha eneo kubwa la Mancheste, alisema: "Jeraha hili lilimwathiri sana mwathiriwa, na hakuweza kufanya kazi wala kusaidia familia yake change.
"Alilazimika kutegemea hisani ya wachezaji wenzake waliolazimika kufanya michango kukidhi mahitaji yake ya kifedha.
"Wakati huo wote, Kerr hajaonyesha majuto yoyote.”
Alisema kukamatwa na kuadhibiwa kwa Kerr ni ishara kwamba “uhuni na ujambazi” katika mechi za kandanda hautavumiliwa tena.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here