IDADI YA MAUZO SOKO LA HISA YAONGEZEKA MARA TANO. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, October 5, 2015

IDADI YA MAUZO SOKO LA HISA YAONGEZEKA MARA TANO.

Meneja wa soko la hisa Patric Mususa.












Idadi  ya mauzo katika soko la hissa (DC) imeongezeka mara tano kutoka bilioni mbili nukta moja hadi kufikia bilioni 12.2 kwa wiki hii.

Akizungumza na wingu la habari jijini Dar es salaam Meneja wa soko hilo Patric Mususa alisema kuwa katika soko hilo pia idadi ya hissa zilizonunuliwa na kuuzwa imeongezeka mara sita kutoka milioni 1.4 hadi kufika  milioni  hadi kufukia milioni 9.1 kwa wiki hii .

Alisema kuwa Kampuni tatu zinazoongoza katika soko hisa zake  kununuliwa na kuuzwa ni pamoja na Baki ya  CRDB inayoongoza kwa 75.35%, TWINGA CEMENT  TPCC ikiwa na  21.81% uko TANAZANIA CIGARETTE TCC ikiwa na 1.38% .

Sanjali na hayo idadi ya mtaji wa soko imeshuka kutoka kutoka trilioni 221.1 hadi trilioni 21.8, wakati idadi ya mtaji wa makapuni ya ndani imepanda kutoka trilioni 9.7 hadi kifikia trilioni 9.8.

Pia mabadiliko ya bei za hisa kampuni  mbili zimeongoza katika ongezeko la bei ya hisa zake ambazo ni TOL imeongezeka kwa asilimia 1.32, NATION MEDIA GROUP NMG kwa asilimia 1.01.

Mbali na hayo Kiashiria cha sekta ya viwanda kimeshuka kwa nukta 55.44 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta ya TBL kwa asilimia 1.19 na TCCL (SIMBA CEMENT) kwa asilimia 2.63 .

Wakati kiashiria cha sekta ya huduma za kibenki na kifedha kimeshuka kwa nukta 28.65 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa kwenye kaunta ya DCB kwa asilimia 2.5 na  NMB kwa asilimia 2.08 na kiashiria cha sekta ya huduma za kibiashara kimeshuka kwa nukta 50 kikiwa kimechangiwa na punguzo la bei ya hisa SWISSPORT kwa hisa asilimia 1.60


Mususa amebainisha kuwa huduma ya kununua na kuuza hisa kwa njia ya simu ya mkononi inaendelea vizuri kwa huduma kwa wananchi wote, nakuwataka watu kuendelea kutumia huduma hiyo kwa kupiga *150*36#.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here