![]() |
| Kaimu Katibu mkuu wa VCCM . |
Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) umewataka
wanachama wa chama cha wananchi CUF visiwani zanziba kuacha vitendo vya
uvunjifu wa Amani katika mikutano ya kampeni za siasa ya chama hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Kaimu
katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa kati ya septemba 15 hadi 18
mwaka huu misafara ya CCM katika maeneo ya Kuyuni, Mtuhaliwa kwa chokocho katika mkoa wa kusini pemba umeshambuliwa
kwa kupigwa mawe wakati wanachama wa CCM wakitoka kuhudhuria mikutano ya kampeni,
na baadhi ya watu wamejeruhiwa na kupata majereha ikiwemo gari moja kuvunjwa
kioo cha mbele.
Pamoja na hayo Shaka amesema kuwa kuhama kwa mwanasaisa mkogwe
Kingunge Ngombale Mwilu si jambo geni kwao kwani tayari walikwisha mvua ukada
mkuu wa jumuhiya hiyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wake katika chama.
Hata hivyo amebainisha
kuwa kuhama kwa Kingunge kunatokana na kutoheshimu matokeo ya michuano ya nguvu
ya hoja ndani ya chama huku akitaka kulazimisha fikra zake zionekane sahihi za
wenzake zikikosa maana na umuhimu wowote.

No comments:
Post a Comment