BONANZA LA SHIMMUTA KUTIMUA VUMBI OKTOBA 10 MWAKA KUU. - WINGU LA HABARI- ONLINE

Breaking

TANGAZO

TANGAZO
Sugar free

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, October 8, 2015

BONANZA LA SHIMMUTA KUTIMUA VUMBI OKTOBA 10 MWAKA KUU.

Shirikisho la Michezo la Mashirika ya umma na makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) zimezitaka  timu zinazotarajia kushiriki bonanza la michezo  Oktoba 10 mwaka huu , kushiriki kikamilifu ili kuleta ushindani katika  bonanza hilo.

Bonanza hilo ambalo limepagwa kufanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuanzia saa 12 asubuhi hadi 12 jioni kwa saa za afrika Mashariki.

Akizungumza na wingu la habari Katibu Mkuu wa SIMMUTA Award Safari  amesema kuwa maandalizi kwa ujumla yamekwisha kamilika na  zitaka timu zote kufata ratiba ikiwemo kufika kwa wakati eneo la tukio .

Safari amebainisha kuwa  mkurugenzi  Mkuu wa  Mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF )Ramadhani   Dau atakuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo.

‘’Siku hiyo ya uzinduzi mgeni rasmi atakuwa Ramadhani Dau ambapo hatazindua bonanza hilo lenye lengo ya kukuza michezo kwani michezo ni afya na inajenga mwili ikiwemo kuepuka magonjwa ya mara kwa mara’’ alisema.

Katika bonanza hilo zinatarajiwa kushiriki Jumla ya timu 10 za taasisi, mashirika ya umma pamoja na makampuni binafsi yaliyopo hapa jijini Dar es Salaam ambapo yatahusisha wanamichezo wafanyakazi wa rika mbalimbali.

Timu ambazo zitashiriki katika bonanza hilo ni pamoja na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari za Tanzania(TPA), Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya(NHIF), Taasisi ya Magonjwa ya Mishipa ya fahamu na Mifupa (MOI), Shirikisho la viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Sanjala na hayo Michezo ambayo itafanyika siku ni pamoja na Mpira wa Miguu, Netiboli, Kuvuta Kamba, Ukimbia ukiwa na kijiko mdomoni kikiwa na ndimu, Kukimbia ukiwa ndani ya gunia, Kukimbia huku ukitunga uzi kwenye Sindano, kula pamoja na kukuna nazi kwa wanaume.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here